WATOA UTHIBITISHO – VI

TAMANI SANA NGUVU KULIKO BARAKA

Mafanikio makubwa ya Ufalme wa Mungu kwa siku za badaye yatakuwa mikononi wa wale tu wanaotafuta jibu la swali hili:

Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

Yohana 6:28

Kanisa la Bwana Yesu limeomba kwa miaka na miaka juu ya kutamani kumuona Mungu kwa kiwango cha juu sana. Na ili kufanikisha hilo wamefanya mikutano mingi ya uamsho, kufunga, mikutano ya hadhara, Matangazo, ushirika, ushirika. Zamani watu walibarikiwa sana, walifurahia uwepo wa Mungu, walicheza katika roho, zilikuwa nyakati kubwa za furaha na baraka.

Tatizo ni kwamba kanisa, mwaka hadi mwaka hadi mwaka, limekwama kwenye baraka tu, na haliingii tena katika uhusiano wa kiroho ambao Mungu ameukusudia! Hatujafika mahali panapotahili. Swali kubwa ni kwa umbali gani unatamani kufika?

Tuna majumba mazuri, mavazi mazuri, tuna misalaba mizuri, tuna madirisha mazuri ya udongo. Tuna kwaya nzuri zenye nyimbo nzuri, tuna ushirika na vyakula vizuri. Tuna watu madhababhuni ambao wameenda seminari kusomea theolojia au wamechukua kozi ya miaka mitatu mpaka minne na wanajua maana ya ibada. Wana uwezo wa kufundisha pointi kwa pointi.

Wanabatiza watoto, wanafungisha ndoa watoto wakikua, wanasikiliza matatizo yao, wanawafuta machozi, wanazika waliokufa. Lakini kuna jambo la msingi sana tena linalohitajika sana! Hayo yote hayatoshi.

HALI HALISI

Jambo ambalo ninakushirikisha leo ni hali halisi ndiyo hali halisi la kanisa la leo.  Hakuna anayependa kujifunza au kusikia mambo mabaya ila ili tuweze kujifunza namna ya kutenda kazi za Mungu, lazima tuyakabili mambo kama yalivyo na si kama sisi tunavyotaka yawe. Lazima tuongee Ukweli hata kama unauma na hata kama unapingana kabisa na kile ambacho tulikiamini maisha yetu yote.

Ni hivi:

Mafanikio yote yanatokana na kujishughulisha na watu, mahali, vitu kama vilivyo na siyo ambayo wewe ungetamani vitu viwe. Kwa kifupi naweza kusema mafanikio ni kushughulika na watu kam walivyo, siyo kama wewe ulivyo.

Hivyo, lazima pia tushughulie hali zote kama zilivyo: Biblia inasema kuwa:

“tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”

Yohana 8:32

UKWELI NI HUU!

Ukweli ni kwamba Kuhusu hali halisi ya kanisa, watumishi na waamini wa siku za leo tupo kwenye tatizo. Na tatizo lenyewe ni kukata tamaa! Yesu alifufuka miaka 2000 iliyopita lakini leo kuna mabilioni ya watu hawamjui Yesu. Hatutaweza kuliondoa tatizo hili kwa kulipuuzia au kusema halipo. Huu ni wakati wa kujipanga na kuzama katika Neno la Mungu ili tuweze kujua hasa mapenzi yake na kusimama imara kama ahadi zake zilivyo kwetu. Lazima tutafute ufunuo mpya, mpenyo mpya ambao utatuingiza katika kusudi la ulimwengu wa roho zaidi ya hali ya sasa.

Hali ya sasa ni ya kushangaza sana, utaona mtu anasema ameokoka bado anakunywa pombe, anasema ameokoka bado mwongo, bado ana mke au mme nje ya ndoa, anasema ameokoka lakini hawezi kujitoa kwa ajli ya kazi ya Mungu. Anasema ameokoka lakini hana hata uwezo wa kumaliza mchawi, magonjwa kila siku ndani yake, umaskini wa kutosha, na woga mwingi. Na mbaya kuna baadhi ya watumishi wanapenda zaidi pesa kuliko kumtafuta ahadi ya Bwana Yesu kwa kanisa.

Kanisa limekosa kweli kubwa sana ambayo Bwana Yesu alifundisha mara zote. Wanalijua Neno, wanauwezo wa kukalili moyoni, lakini wamekosa Ukweli hali wa hilo Neno, kile ambacho Neno linaweza kufanya na Roho Mtakatifu na hili ndilo limekuwa “bomu” la kiroho.

Ni wazi katika Neno, Bwana amekusudia kwamba kanisa liwe na nguvu ya Roho Mtakatifu ili kuweza kuufikia ulimwengu, lakini kanisa limekosa hii nguvu tena pakubwa.

Yesu alipotuahidi kwamba tutapokea Roho Mtakatifu, hajawahikutuahidi kwamba tutanena kwa lugha tu. Zoea kuwa na nguvu! Nenda zaidi ya kiwango cha baraka na uingie katika kiwango hatma ya kinabii ya Mungu kwa ajili ya kania lake. Kuna zaidi ya katika Pentekoste kuliko kushika elimu tu. Kuna kuzeoa Nguvu. Maana ukizoea kuwa na Mungu utashinda hata ukikutana na Farao na ukatoa tamko “Bwana wa Isareli aseme, ruhusu watu wangu waende!”.

Tunatakiwa kuwa na kiu hasa ya kuwa na nguvu za Mungu kuliko hata unavyotamani kubarikiwa. Yesu hakuwaambia wanafunzi wake wasubiri pale Yerusalemu mpaka wapokee baraka, au kipiwa cha kunena kwa lugha. Aliwaambia:

“…mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu…”

Matendo ya Mitume 1:8

Walikuwa wanangoja NGUVU ya Roho Mtakatifu! Siku za leo watu wamekuwa wavivu sana kungoja mbele za Bwana. Wengi wamekwama kabisa kuvuka kiwango cha kutamani baraka na kufikia Ahadi ya Bwana Yesu. Ahadi ya Bwana Yesu ni NGUVU.                                                                                                    

🗣 OMBA:

  1. Omba Mungu akupe neema ya kujiliwa na nguvu ya Mungu ili uweze kuleta maana katika ufalme wa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo. Amina!

Unaweza kujiunga kwenye group la Goodvine Discipleship School la WHATSAPP kwa kujaza fomu hapa chini:

http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36 AU Tuma meseji kwenye namba 0752122744 Ikiwa na jina lako na mkoa unaoishi.

WATOA UTHIBITISHO

SISI TU WATOA UTHIBITISHO

Matendo ya Mitume 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Roho Mtakatifu anakuja juu ya maisha yetu kwa kusudi. Ametolewa na Bwana Yesu kwetu waamini kwa ajili ya ulimwengu. Ubatizo wa Roho Mtakatifu sio kwa ajili ajifurahisisha kwetu au kubarikiwa tu. Kuna wajibu ambao tunapaswa kuutekeleza kulinana na vipawa vya Roho Mtakatifu ulivyopewa.

Kazi za Mungu zinafanywa kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu pekee.

Yesu analiweka sawa hili anaposema tutapokea nguvu, au uwezesho, Roho Mtakatifu atakapotujilia juu yetu. Ukweli hasa hili ni kwamba nguvu itatufanya kuwa watoa uthibitisho wa Neno la Mungu kwa watu wa mataifa (wasio-okoka) kwamba Yesu yu hai. Tumeitwa tumeteuliwa na kuwezeshwa kama mashahidi rasmi wa Bwana Yesu kupitia uwezesho wa Roho Mtakatifu.

Wazo kuu

Yesu kupitia kwa Roho Mtakatifu, ametoa ahadi ya kukuwezesha na kukupa uwezo usio wa kawaida ili uweze kutoa uthibitisho kwamba Yu hai. Na hili ndilo kusudi kubwa la Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Uwezo wote wa kiungu, uwezo usio wa kawaida wa Roho Mtakatifu umeachiliwa kwetu ili tuweze kufanya kazi ya ushahidi.

📖 Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”.

Hatua za uanafunzi.

Kuna hatua tatu za msingi ambazo zinatimizwa ndani yako pale Roho  Mtakatifu anapokuwezesha uweze kuwa mtoa uthibitisho wa kwamba Yesu yu hai. Kwanza, anakupa uwezo wa kunena Neno la kweli lenye nguvu kwa kuhubiri injili kwenye maisha ya watu. Pili, anangára maishani mwako kupitia uwepo wake ili Kristo aonekane kupitia wewe. Tatu, Roho Mtakatifu anakupatia vipawa vya mawasiliano kupitia ishara, miujiza na maajabu. Haya ni maisha ya kweli, ambayo Mungu anataka ukue katika hayo kama mwanafunzi wa Kristo.

Soma: Matendo 1:4-8

🗣 TUOMBE

  1. Asante Roho Mtakatifu kwa matendo yako ya ajabu ndani yangu, na kwa kunisaidia niweze kutenda mambo makuu, katika Jina la Yesu, Amina.
  2. Ee Bwana, napokea uwezo wako wa kiungu ili kuuthibithishia ulimwengu kwamba uko hai na ni Bwana wa wote. Nijaze kwa upya leo kwa ajili ya kazi inayoendela. Ruhusu dunia ikuone WEewe ndani yangu ttangu sasa, katika Jina la Yesu nimeomba.

Unaweza kujiunga kwenye group la PASTORBON WhatsApp kwa kujaza fomu hapa chini: http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36