KIONGOZI MTUMISHI

Soma zaidi:  YOHANA 13:13-17
Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.

UJUMBE
Moja kati ya tofauti kubwa kayi ya viongozi watumishi na wanaojitumikia ni kwamba, hawa viongozi watumishi muda wote wanauona uongozi kama tendo la huduma, na hawa viongozi wanaojitumikia wanauona uongozi kama cheo na wanatumia muda mwingi kuhakikisha wanalinda vyeo vyao. Viongozi watumishi wanakumbatia na kukaribisha maoni, wakiona kama ni chanzo kikubwa cha taarifa za namna gani wanaweza kutoa huduma bora, lakini wale wanaojitumikia muda wote hujibu hasi au vibaya na wakichukua maamuzi mrejesho usioumiza kama ishara ya kukataa. Katika Mathayo 20:26b-28 Bwana Yesu alisema;

“ Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.”

Kutumikia wengine ni utumishi kwa wengine. Si jambo la madaraka ya ushawishi, au nguvu ya siasa. Badala yake, ni kutafuta fursa ya kutumikia wengine. Wala si jambo kuvutia watu ili wakusikilize. Uongozi wa kutumikia wengine unakuwa si wa kuigiza na mara nyingi jnatumika kwa namna isiyotabirika. Mambo madogo tu yatakufanya uwe kiongozi mtumishi wa watu. Yaweza kuwa kuokota takataka nyumbani au kanisani au ofisini kwako, au kiongozi unapika chai kwa ajili wa watumishi ofisini.

Hakuna kazi yenye kipato zaidi kwa kiongozi mtumishi; kuna jambo kubwa zaidi ya tabia inayomtofautisha kiongozi mtumishi. Ni nia ya kutamani wengine wafanikiwe. Anatambua kuwa wale wanaomzunguka wakifanikiwa, basi kuna nafasi kubwa sana ya kwamba na yeye ataona mafanikio. Ana hekima ya kutamani kilicho bora kwa ajili ya wengine.

Bwana Yesu alitumika kwa utukufu wa Mungu. Kwa kiwango cha juu kabisa utumishi wake alishusha maisha yake chini kwa upendo. Katika Mathayo 10:39, Bwana wetu Yesu ambaye ni mfano wa kiongozi mkamilifu alisema;

” Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.”

Kiongozi yeyote ambaye ambaye amejazwa na vipaumbele vyake vya kibinafsi, kulinda hadhi yake, na kutunza nafasi kwa manufaa yake, huyu hataweza kuwa balozi mzuri wa Yesu.

Jambo lingine litakalokusaidia kuwa huyu ni kiongozi mtumishi ni maadili. Daima utawakuta ni watu waliojawa na maadili. Mithali 11:3 anasema:

“Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.”

Hivyo anakuwa ni mtu anayetaka kumpendeza Mungu muda wote, kuna mambo hawezi yafanya. Chochote ambacho Mungu hapendezwi nacho naye hafanyi.

Ni mtu mwadilifu, ana kawaida ya kufika muda uleule ambao umepangwa kuwapo ofisini. Uhalisia ni kwamba wale walio chini yake watawahi kufika kabla yake maana wanajua kiongozi wao hana mzaha na muda. Hawezi pindisha ukweli. Hatanunua kitu cha shilingi 6,000 na akasema amenunua kwa shilingi 10,000. Anatunza sana ahadi zake. Neno lake ni kifungo chake. Mahusiano yake na jinsia tofauti ni safi. Hawezi kuchukua kitu kisicho chake. Ana mikono safi na moyo safi. Je wewe ni mtu mwenye maadili?

Pointi ya kuomba.
Baba, nifanye kuwa kiongozi mtumishi wa wengine. Daima nizingatie kanuni zako za mahusiano katika Jina la Yesu.

Mungu akubariki.