MWAMINI MUNGU HATA ASIPOJIBU

Soma Biblia Yote kwa Mwaka Mmoja

Mathayo 15:22-23 (SUV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²² Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.

²³ Wala yeye hakumjibu neno…

Soma zaidi: Sefania 3:17
“Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.”

UJUMBE
Inawezekana ni mwana wa Mungu unayesoma maneno haya, yawezekana umejaa huzuni, maswali na kila namna ya kuvunjika moyo, mapigo ya moyo yanakutwita kwa sababu upo katika gali ambayo hukuitarajia. Unatamani kuisikia sauti ya Bwana Mungu “uwe na amani”, lakini ukimya na usiri wa kushangaza japo unaniuliza Mungu maswali mengi – “Hakumjibu Neno lolote.”

Moyo wa huruma wa Mungu lazima uume kusikiliza huzuni za watu wote duniani, malalamiko, vilio ambavyo vinainuka kutokana na udhaifu wetu, mioyo isiyo na subira, kwa sababu hatuoni mapenzi yetu yakijibiwa. Hana kawaida ya kujibu kila kitu ambacho macho yetu yanaona au tunachokitolea machozi.

Ukimya wa Yesu ni wa maana kama kauli yake ilivyo ya maana, unaweza kuwa ni ishara, haimanishi kwamba hajakukubali, bali anakukubali na ameamua kunyamaza kwa kusudi na baraka kwako.

Kwa nini unainamisha chini roho yako? Unapaswa kumshukuru Mungu hata akikaa kimya. Sikiliza hadithi hii ya binti wa zamani ya namna ambavyo Mkristo mmoja aliota kwamba aliwaonya wengine watatu katika maombi. Walipokuwa wamepiga magoti Bwana Yesu akasogea karibu nao.

Alipomsogelea wa kwanza, Aliimwinamia kwa unyenyenyekevu na upendo, akitabasamu na kumuonesha upendo na akaongea naye kwa kilugha, uwazi na raha sana n.k

Akamwacha akaamwendea wa pili, lakini aliweka mkono wake tu juu yake na huyu msichana akainamisha kichwa, alimtazama tu kwa kumkubali.

Kwa mwanamke wa tatu, alipita haraka, bila kusimama kwa Neno lolote wala salamu. Huyu mwanamke aliyekuwa anaota akajisemesha “Basi anapenda sana wa kwanza, na wa pili pia anapenda kiasi, ila huyu wa tatu hajamfanyia chochote cha kuonesha upendo kama kwa yule wa kwanza; na huyu wa tatu alihuzunika Sana kwa sababu hajaambiwa chochote na hata jicho la upendo halikuwepo.

“Ninashangaa sijui kafanya nini, kwa nini Bwana ameonesha tofauti sana kwa wote watatu?” Akiwa anatafakari hayo, Bwana mwenyewe akatokea pembeni yake na kusema: “Ewe mwanamke! Mbona umenitafsiri vibaya. Yule mwanamke wa kwanza anahitaji msaada wangu wote na nimjali Sana ili aweze kupita kwenye njia nyembamba. Anahitaji upendo wangu, mawazo yangu na msaada wangu kila saa. Bila hivyo atashindwa na kuanguka.

“Wa pili, ambaye nilimtazama na kumwacha, anayo imani na anajiamini ingawa mambo yanaweza kubadilika na akafanya chochote ambacho watu hufanya”

“Yule wa tatu, ambaye nilionesha kutomwangalia, na nikamwacha, anayo imani na upendo ya kiwango bora, ninamfundisha haraka hatua za kufanya makuuu na utumishi Mtakatifu.”

“Ananijua vizuri na ananipenda kwa dhati na kuniamini kupita kawaida ya wanadamu. Haitaji mpaka nimfanyie kitu kujua nina mpenda, hana shida na havunjiki moyo kabisa kwa jambo lolote Yeye anafaulu mtihani wa kipimo cha upendo wake kwangu. Nimeshapanga kwamba atashinda duniani na Mbinguni ataingia; kwa kuwa ananiamini mimi kiasi kwamba hata akili yake ikikataa, moyo wake unaweza mshawishi kuniasi lakini huyo wa tatu hawezi kuniacha kamwe; – kwa sababu anajua ninachofanya kwa ajili ya ukulele wake, na kwamba ninachokifanya hahitaji maelezo leo, ataelewa hapo badaye.

“Nimemnyazia mpenzi wangu kwa sababu ninapenda zaidi ya nguvu ya maneno ya wanadamu yanaweza kueleza, au namna moyo wa mwanadamu unavyoweza kuelewa. Akaniambi ” kwa faida yako, pia jifunze junipenda katika roho, pasipo kunipenda huku unataka kitu fulani kwa sababu unajua ninacho.””

Bwana “atatenda makuu kwako” ukiamua kujifunza siri ya ukimya wake, na ukamsifu daima, kwa maana hivyo ulivyo na pumzi uliyonayo ni zaidi ya unavyotamani. Subiri kwa upendo, asianze mengine kwa sababu Bwana amenyamaza. Anawajua waliowake na anatuwazia mema daima. _ Ndilo fungu langu.

DOKEZO
Mpende Mungu hata kama hajafanya unachotaka akufanyie.

Unaweza kujiunga Telegram kwenye group la Pillars of Destiny ili kupata masomo haya kila siku.

BAADHI YA WATU HUJA KATIKA MAISHA YAKO KAMA BARAKA, BAADHI KAMA MASOMO TU.

Kuna mambo mengi sana ambayo ni muhimu kuyajua katika maisha na kujua aina mbalimbali za watu, kujifunza namna ya kuwasoma wanadamu, na kujua namna ya kutofautisha kati ya kuwa na watu wanaotufaa na wasio tufaa. Ni bora na muhimu sana kujiweka karibu na watu wa aina zote na kujua huyu ana akili gani na huyu ni wa aina gani kwa kuangalia utu wao, tabia zao, mwenendo wao, matendo yao na jinsi wanavyoweza kupambanua mambo. Ni muhimu kujua hili, baadhi ya watu huja katika maisha yako kama Baraka kwa kuwa wanakufaa sana katika maisha na wa kweli kwa kwako, kamwe hawawezi kukudanganya na kamwe hawawezi kukusaliti ama kukuondolea imani nao, hawa siku zote ni kama uti wa mgongo wako , ni sehemu ya maisha yako na huishi nawe bila ya kutafutiana au kuwekeana madoa.

Lakini kuna baadhi ya watu huja katika maisha yako kutoa somo tu, wakati mwingine urafiki, mahusiano vinaenda tofauti na vile ulivyo tarajia ama kukusudia katika maisha yako kutokana na kundi hili la watu na hapo ndipo swala la kujifunza linakuja. Kwani utaona rangi halisi ya mtu , utu halisi wa mtu, mwenendo halisi wa mtu na tabia yake halisi hujitokeza muda huu. Hatua hii ndipo utawajua watu na baadhi ya watu wana karama (gift) kuwasoma wenzao papo kwa papo na kujua huyu ni mtu wa aina gani kwa kuangalia tu baadhi ya mambo kama vile, macho, jinsi anavyoonesha sura yake na matendo halisi ya mwili wake kama vile kujitikisa, geuka geuka n.k hapa waswahili wanaita –body language.

Vitendo vya mtu na macho yake vinaonesha sana kuwa huyu ni mtu wa namna gani? Naona unajiuliza Boniface anaongea nini hapa… nasema hivi, kuna watu wana uwezo wa kumtazama mtu maramoja na wakaeleza mambo ambayo mtu mwingine kamwe hawezi kuyaona hata iweje. Sote tunatakiwa kujifunza namna ya kuwasoma watu na kuwa wahukumu wazuri wa tabia za watu. Ukijifunza hili litakusaidia sana katika maisha yako ya kila siku na yajayo katika kutengeneza marafiki, mahusiano na mambo mbalimbali yanayohusiana na kushirikiana. Ni muhimu sana kuwa makini kabla ya kumwamini mtu na kumpa moyo wako wote, ufahamu wako wate na roho yako pia. Ni rahisi sana kudanganywa na watu ambao wao wanauwezo mkubwa wa kudanganya kwa mambo ambayo tunatamani kuyasikia na wanajaribu sana kukonga nyoyo zetu kwa kubadili akili zetu na mitazamo yetu, kumbuka hutumia mbinu za ziada au triki kali sana. Kujifunza mambo ya muhimu katika maisha ni jambo la muhimu sana, itatusaidia kukua, itatusaidia kwa matatizo yasiyoisaha yanayoweza kujitokeza muda wowote, na hata mambo mapya katika maisha ambayo yulikuwa bado hatujayakabili au kuyafikia. Kuna aina zote za watu katika dunia hii; kuna tabia nyingi sana na mambo mengi kutokana na mazingira halisi. Kwa kadri unavyojinza zaidi ndivyo tunavyozidi kuwa na uwezo zaidi wa kukabiliana na watu, kukabiliana na hatua mbalimbali za ukuaji wa mtu katika maisha yetu. Tunatakiwa kujifunza kutokuamini haraka na kujifunza kutokutoa kwa asilimia mia moja vinginevyo utoapo asilimia mia moja zako uwe na uhakika na kile ukifanyacho. Wakati mwingine maisha yanaweza kuyeyusha kitu kigumu, lakini tunahitaji kuwa imara na tunahitaji kufunga kurasa mbaya tulizopitia na kufungua kurasa safi kwa umakini.

Ndugu zangu, Maisha matamu sana lakini mafupi mno. Kila jambo hutokea kwa sababu fulani, iwe nzuri ama mbaya lakini ni sababu murua, kuna watu wanakuja katika maisha yako na wengine wanatoka kutoka na sababu mbalimbali. Sote tupo katika njia tofauti katika maisha na muhimu zaidi ni nani tunamchukua kuwa nasi katika hii safari na nani tunashirikiana naye naye au nao pamoja. Kuwa na furaha, kuwa na mtazamo chanya, jasiri, mhalisia wa maisha. Kama mambo ni magumu, yanayumba na yanakusononesha kwako sasa, siku zote kumbuka kuwa hakuna masika yasiyo kuwa na ncha. Mungu yupo siku zote kutulinda na kututazama kwa msaada. Kujifunza masomo muhimu tunayopitia katika maisha ni jambo ambalo litakusaidia sana katika maisha ya usoni au mbeleni. Japokuwa mara nyingi hawaamini kama ipo siku wakao-nyookewa kwa matumaini kidogo, mambo makubwa huja kwa uvumilivu, ustahimilivu na maono ya kimikakati. Tunapotegemea na kuendelea kutegemea, ianaweza kuchukua muda nab ado matokeo yakawa tofauti na matarajio yetu. Usikae unatafakari mategemeo yako muda wote, wewe fanya kazi, soma, n.k usijitie nuksi (don’t jinx yourself) usijikandamize mwenyewe na mawazo. Acha watu wazuri katika maisha yako waje kwa nguvu ya asilia au naturall. Hakika Mungu atakuweka katikati ya kundi la watu wema na kila kitu kitakuwa sawia kwako.

Najua fika muda mwingine mambo hayaleti maana kabisa kwa namna gani maisha yako yalivyo au watu ulionao karibu. Tunahitaji kuwa watu wa mtazamo wa mbali na kujikita katika kufanya kazi au kusoma alama za nyakati. Fanya lisilowezekana, liwezekane bila majuto, hakuna kurudi nyumana fanya kile ambacho ni bora kwako wewe ili kupata raha yako mwenyewe na ndoto zako na matakwa yako yatimie. Lazima itokee yatimie, penye nia pana njia siku zote na kwa kila jambo. Anza kujaribu, kwa muda mfupi utaona mabadiliko. Usiogope, kuwa na furaha na endelea kusongesha gurudumu lako la maisha.

Kama somo hili linaeleweka basi nitie moyo kwa kusema asante ukisoma na kama halieleweki uliza ntafafanua nikitulia..


   Mwandishi wa makala hii anapatikana pia:

fb Facebook        twitt  Twitter           link LinkedIn