Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu

Zaburi 105:15

SOMA ZAIDI: 2 WAFALME 1:1-18

1 Ikawa, baada ya kufa kwake Ahabu, Moabu wakawaasi Israeli.

2 Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu.

3 Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?

4 Basi sasa, Bwana asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka.

5 Wale wajumbe wakarudi, na mfalme akawaambia, Mbona mmerudi?

6 Wakamwambia, Mtu alitokea, akaonana nasi, akatuambia, Enendeni, rudini kwa mfalme yule aliyewatuma, mkamwambie, Bwana asema hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.

7 Akawaambia, Je! Mtu yule aliyetokea, akaonana nanyi, akawaambia maneno hayo, alikuwa mtu wa namna gani?

8 Wakamwambia, Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema, Ndiye yule Eliya Mtishbi.

9 Ndipo mfalme akatuma akida wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka.

10 Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.

11 Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.

12 Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.

13 Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.

14 Tazama, moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako.

15 Malaika wa Bwana akamwambia Eliya, Shuka pamoja naye; usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa mfalme.

16 Akamwambia, Bwana asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.

17 Basi akafa, sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana.

18 Na mambo yote yaliyosalia aliyoyafanya Ahazia, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?

UJUMBE

Mambo ya kuzingatia unapoutafuta uso wa Bwana

 1. Uswaguse wapakwa mafuta
 2. Usiwaguse wanaobeba Ujumbe wake
 • Ingawa upako ulio katika mpakwa mafuta unaweza kuleta matokeo mazuri kwenye maisha ya watu, lakini pia unaweza kuleta madhara mabaya sana kwa wale wanaotukana mpakwa mafuta au kumfanyia vibaya au kuishi naye kwa chuki.
 • Roho Mtakatifu anatupa onyo katika Zaburi 105:15 ili tuweze kujizuia kuyatenda hayo mwisho wetu ukawa mbaya. Hili linanikumbusha mtu ambaye alikuwa kiongozi baadaye akawa kinyume na Mchungaji wangu kiongozi Philipo James Guni, kwa huzuni kabisa alikufa na vidonda kichwani.
 • Hilo ni sawa na habari mbaya ya Mfalme Ahazia wa Samaria, ambaye alijaribu kunyoosha mkono wake kwa Eliya alipata ugonjwa na akaamua kutuma watu kwenda kumuuliza Mungu wa kigeni kama atapona. Je, kosa la Eliya ni lipi? Maana Mungu alimtumia alie akamuulize kuwa mpaka unaamua kutafuta matibabau kwa mungu wa kigeni, Mungu wa Israeli hayupo?
 • Kwa sababu Mfalme alikuwa kinyume na amri ya Bwana ya Kumbukumbu la Torati 18:10-11 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.”
 • Onyo la Mungu mara zote likisikilizwa, linapelekea msamaha, kama tuonavyo katika Yona 3:10 “Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende”. Hapa tunaona Mungu amegeuza hasira ya kutaka kuiangamiza Ninawi na wakasamehewa kwa sababu walikubali kosa.
 • Cha kushangaza pale ambapo tunaona Mungu kamtuma Mtumishi wake awarudishe wale maaskari ili kumwokoa mfalme lakini hatutaka kusikia akaagiza Mtumishi huyo auwawe?
 • Je, Mchungaji wako anapokufundisha au kukuonya au kukukaripia ili tu akufikishe mahali pa toba na Ukombozi wako wa sasa na uharibifu Wowote usikupate, unajisikiaje?
 • Tunaona maamuzi ya kijinga ya mfalme yanapelekea msiba sio tu kwake, bali pia kwa maaskari 102.

Tunajifunza nini na tuombeje?

 1. Lazima tuwaombee viongozi wetu wabaya kwa sababu Mungu atapoamua kuhukumu hata wasio na hatia wanaweza wasipone.
 2. Wana wa Mungu wakati wote watambue kuwa kila jukumu wanalopewa liwe la Mungu au la nani wanatakiwa kuomba hekima ya kulitendea kazi.
 • Watumishi wa Mungu wanatakiwa muda wote kuishi maisha ya utakatifu ili kwamba mafuta ya Mungu yaweze kuwapigania kwa niaba yao.
 • Kwa yeyote ambaye amewahi kumdharau Mtumishi wa Mungu uwe makini, usije ukapitia madhara mabaya ya upako.

OMBI:Kama umewahi kumtendea kwa chuki Mtumishi wa Mungu au kunena vibaya, tubu na uombe msamaha na Uponyaji wa Mungu.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s