USOMAJI WA BIBLIA KWA MWAKA MMOJA

Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi

Kifo ni dalili ya kukatika kwa kila aina ya uhai. Inaweza kuwa ni mauti imeingia katika afya, kazi, elimu, ndoa, wazo, au biashara ya mtu. Popote ambapo nguvu ya mauti inajitokeza, daima inapelekea kukomesha, kutokomeza, adhabu, uharibifu, kuanguka kabisa na kupoteza matumaini. Mauti ina nguvu sana kiasi kwamba imetangazwa kuwa ni adui wa mwisho kuangamizwa;

I Wakorintho 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.”

Ashukuriwe Bwana Yesu kwa kumwangamiza aliye na nguvu ya mauti, sasa Yesu ndiye ameshikilia ufunguo wa mauti, ili kwamba kamwe mauti isije kuwatesa walio wake (Waebrania 2:14, Ufunuo 1:18).

Ezekieli 37:1-10

Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele

NAMNA YA KUINUKA

Tambua Yesu anakupenda

Luka 4:18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa.

Iamini injili (kaa katika Neno)

Zaburi 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

Neno ni uhai. Neno likikaa ndani ya mtu, linaweza likamfanyia yote anayotaka, maana ndani ya Neno kuna kila kitu anachotaka.” Unachohitaji zaidi ni utii wa Neno. Neno ndilo linaweza kukutakasa maana neno ni Injili. Injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye (Warumi 1:16)

Endelea kumtumikia

Kumtumikia ni njia pekee inayo ruhusu baraka ikujilie kwenye maisha yako. Kwa kadri unavyozidi kilindenda hilo Neno, ndivyo utakavyoingia kutoka utukufu hadi utukufu. Jinsi utakavyokuwa unatekeleza, ndivyo utakavyokua unaondoka kutoka mautini na kuingia katika uzima. Ndivyo utakavyozidi kusonga mbele, ukitii neno, yaani hilo KUSUDI, ndivyo utakavyokuwa unatakaswa, na kuinuliwa na kubarikiwa, na kutengwa na kufanywa imara siku kwa siku katika utakatifu wa MUNGU, hata kufika cheo cha KRISTO, kwa maana hilo neno limekusudiwa kukufikisha wewe katika cheo cha KRISTO.”

Tabiri habari njema (baraka zako).

Hapa ndipo heshima na nabii inapojitokeza. Kila aliye wa Yesu ni nabii maana imeandikwa

Mdo 3:25-26 “Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. 26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.”

Injili maana yake habari njema. ‘utaenda Jehanam’ hii siyo habari njema. Yesu alikuja kubariki watu wake na sio kuwalaani, hivyo nami nimekuja kwenu kutimiza baraka ya Kristo (Warumi 15:29).

Je unapitia mauti katika eneo lolote maishani mwako? Ufufuo na uzima anasema kwako leo: inuka!

Omba: Baba, haribu nguvu ya mauti ndani yangu na unipe uzima wa milele katika Jina la Yesu.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s