Hiki ni kiwango kingine cha imani.

Leo tunapaswa kusoma Mambo ya Walawi sura ya 14 yote.

Imani kubwa daima itatafuta njia inayoitaka au matarajio yake, daima itakufanya uwe mtu wa kuamuru. Mungu anatuonesha njia ya kufikia imani kubwa. Kiwango cha imani yako kitaleta majibu ya kiwango cha matokeo, imani haba itakupa matokeo haba, lakini imani kubwa itakupa matokeo makubwa.

Imani kubwa daima itakufanya uwe mtu wa amri, kwa sababu tayari umeshaijenga imani yako kwa kiwango ambacho unaanza kutenda kwa roho wa imani; kama ilivyondikwa;

Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena;

2 Wakorntho 4:13

Huwezi kuendelea kubaki na kiwango cha imani ulichonacho, au kubaki na imani haba uliyonayo. Unao wajibu wa kuendelea kuijenga imani yako mpaka ikue na kufikia kiwango cha imani ya kanisa la Thesalonike, ambalo imani yake ilielezwa kuwa “imani yao ilizidi sana.”

 Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.

2 Wathesalonike 1:3

Imani kubwa inakufanya uwe na amri juu ya chochote, wakati roho ya imani inakuimalisha.

Mungu anataka kila mmoja wetu akue katika kipimo cha imani (Warumi 12:3). Mungu hapendi kuona mtu yeyote anadumaa. Anataka kukuona una KUA katika Yeye. Kukua katika Yeye ina maanisha kwamba kukua kutoka imani hata imani (Warumi 1:17). Hii ina maanisha kumjua Yeye zaidi na zaidi, kumjua Mungu zaidi wiki hii kuliko wiki iliyopita. Kumjua zaidi leo kuliko jana.

Zifuatazo ni njia nne za kukuza imani yako

1. Kusikia Neno

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Warumi 10:17

Kama unataka kukuza imani yako, jambo la kwanza ni kusikia, na hii ina maanisha kwamba jifunze kujilisha mwenyewe Neno la Mungu. Unapolikia Neno la Mungu, linakubadilisha. Linabadilisha mtazamo wako na namna unavyowaza inabadilika. Linaosha ubongo wako (Yohana 17:17).

Tunatakiwa kuviona vitu kwa namna Mungu anavyoviona, tunapswa kuwaza kama Mungu anavyowaza. Habari njema ni kwamba kipo kitabu ambacho kimejaa tu habari za namna Mungu anavyowaza: Biblia. Fungua Biblia yako anza kusoma, sikiliza mafundisho ya Mtumishi wa Mungu mwenye Roho wa Mungu ndani yake. Kwenye gari lako jaza mahubiri kuliko miziki ya kidunia n.k

2. Kuliamini Neno

Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]

Matendo ya Mitume 8:37

Ni jambo moja kusikia Neno … na ni jambo lingine kuliamini hilo Neno. Unaweza kuwa umesikia kwa miaka mingi sana kuwa Yesu ni Bwana. Lakini siku utakapoliamini hilo Neno utaanza kuona ukuu ya Yesu maishani mwako.

Warumi 10:9-10 inasema, “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Umefanyika Mkristo kwa kusikia na kuliamini Neno. Jambo kama hilo limefanyika kwenye maisha yako yote, unapaswa kujua Mungu amesema nini na ukaamini hicho hata kama mazingira au hali yako hairuhusu wewe amini ahadi za Mungu pakee. Unaposoma Neno la Mungu usisahau kuliamini. Mfano Neno linasema:

  • “Mimi ndimi Bwana nikuponyaye” (Kutoka15:26).
  • “kwa kupigwa kwake mliponywa.” (1 Petro 2:24).
  • “[Yesu] akawaponya wote” (Mathayo12:15).

Kama Neno la Mungu limesema, hilo jambo limekwisha. Ni wakati wa kuliamini Neno.

3. Kuongea Neno

Mtu yule akaniambia, Mwanadamu, tazama kwa macho yako, sikia kwa masikio yako, ukaweke moyoni mwako, yote nitakayokuonyesha; maana umeletwa hapa kusudi nikuonyeshe haya; tangaza habari ya yote utakayoyaona kwa nyumba ya Israeli.

Ezekieli 40:4

Unaweza kusema “Ila bado naumwa”

Ukishasikia Neno la Mungu na ukafanya maamuzi kuliamini, unatakiwa kufanya maamuzi ya kulichukua. Ichukue hiyo kweli na kamwe usiruhusu iondoke.

Ukisha sikia na kuamini Neno tunasema kwamba umeuona uzuri wa Mungu, tangaza hilo, ongea hilo. Ukiona unaumwa na ukaona Neno la Mungu linavyosema juu ya magonjwa, unatakiwa kuchukua hayo maneno, andika mahali, shika kichwani na utangaze sawasawa na hilo Neno na si hali yako. Ongea hayo kila siku.

4. Kufanya sawasawa na Neno

Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

Yakobo 2:17-18

Kusikia, kuamini na kulitangaza Neno hakutoshi – chukua hatua zaidi ya kiimani. Kama unaumwa na umesikia Neno la uponyaji, ukaamini na umeanza kulikiri au kulitangaza, kuna hii hatua muhimu sana kwakoni kuamka asubuhi na kuanza kumshukuru Mungu kwa uponyaji hata kama bado unasikia maumivu. Unashukuru kwa kile unachoamini. Kitendo cha kufanya hivyo kinaonesha ukomavu wa imani yako.

Kusikia. Kuamini. Kutangaza. Kutenda. Ukimsikilza Bwana, amini anachosema, anza kusema kama alivyosema na tendea kazi hicho, utajikuta unakua kiimani kuliko wakati wowote hapo nyuma. Neno la Mungu litafanya kazi ndani yako kuliko kitu chochote na utaishi maisha ya IMANI kubwa.

One thought on “VIWANGO VYA IMANI – III

  1. Nimebarikiwa sana na mafundisho yako, naornda jinsi unavyotumka kiswahili kizuri na kinaekeweka kinampa msomaji kupoke.
    Somo ni zuri limejaa nguvu ya Mungu
    Ubarikiwe sana.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s