USIOGOPE

USIOGOPE

Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
ISAYA. 43:1

Wakati mwingi katika maisha tunayoishi vimejitokeza vitisho ambavyo vinamfanya mtu aanze kuogopa au kutishika kuthubutu kuanza Jambo alilokusudiwa kufanya na Mungu.

Ukiona wazo lolote limekuja kichwani mwako na hilo wazo linaoneonekana kutokana na Neno la Mungu tambua unapaswa Kulifanya Tena kwa viwango vya ubora wa hali ya juu.

Si jambo rahisi kabisa kutekeleza jambo ambalo litakupa kumfurahisha Mungu, kufurahisha watu na familia yako. Hapo ndipo vitisho vilipojificha na vinakusubiri uanze au ujaribu kugusa hilo.

Utaanza kusikia kelele za mawazo yako na wanadamu, kelele zote zinakusudia kusema huwezi, usijaribu, acha, utapoteza muda, ukishindwa, shauri yako na maneno yanayofanana na hayo.

Mimi Mchungaji Boniface nakuambia hivi tazama hili Neno la Mungu linasema;

Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.

Ee Yakobo (kwa Mimi nasoma hivi Ee Boniface) na anaposema Ee Israeli (Mimi nasoma hivi Ee mpendwa wa Mungu). Nisiogope kufanya jambo ambalo linatokana na maono niliyopewa na Mungu hata Kama Kuna uzito kiasi gani.

Inawezekana wewe sio mtu wa kuajiriwa bali unatakiwa uanze Jambo ambalo litawatengenezea wengine ajira. Uanze jambo ambalo hakuna hata mmoja amewahi kufanya katika familia yenu.

Bwana anasema amekuita kwa jina lako, nikuambie hivi acha woga, simama ukijua Bwana amekukomboa ili ufanye mambo makuu na sio ya kawaida kawaida kama ambao hawajakomboa na bado hajawaita.

TANGAZA:
Mimi nimekombolewa na Mungu kwa damu ya Yesu Kristo pale msalabani, sizuiliwi Wala kuogopa chochote maana nimeitwa na Mungu na nimefanyika kuwa Mali ya Mungu. Sitashindwa wala kukata tamaa kamwe kutimiza ndoto yangu.

J!Boniface Evarist
GoodVine Church.
+1 619 800 1920
+255 752 122 744