BWANA ATAKURUDISHIA AFYA

“Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao.”

Zaburi 147:3

Agano jipya limejaa matukio mengi ya watu ambao waliponywa, lengo kubwa ni kutushawishi sisi kwamba uponyaji unawezekana kupitia Yesu Kristo. Zipo fadhila, utukufu na nguvu ya ajabu sana ndani ya jina la Yesu. Kila aliyewahi kukutana na Jina hili au Nafsi yake hakuwahi kubaki alivyokuwa, haijalishi ukubwa au udogo wa kiwango cha ugonjwa waliokuwa nao. Kila kitu kinawezekana kupitia Jina la Yesu. Tunasoma;

akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye

Kutoka15:26

“Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana”.

Mathayo 19:26

Kupitia Jina la Yesu kuna nguvu kubwa sana ya kushinda kila aina ya maradhi na magonjwa.

“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;-

Wafilipi 2:9-10

Endapo utatambua kuwa Yesu alilipa gharama zote kwa ajili ya ukombozi wetu ili tuwe huru dhidi ya kila magonjwa, ndipo utaweza kukubali kwa ujasiri kuwa Bwana Yesu ndiye chanzo cha uzima wetu. Kupitia wokovu Bwana Yesu ametupatia; uzima, afya, amani na vingine vingi kwa wingi. Yeye mwenyewe alichukua maumivu yetu na akabeba magonjwa yetu. Mara zote anatamani kufanya vitu ili kulithibitisha Neno lake, na ili tutambue kipimo cha mawazo ya Mungu juu yetu.

Kama unauhitaji wa muujiza mmoja wa uponyaji au jambo linguine, au umeteseka na maumivu ya magonjwakwa muda mrefu, Bwana Yesu atadhihirisha ukamilifu wa utakaso na nguvu ya uponyaji katika maisha yako. Unachohitaji ni kuwa ina Imani kwake tu. Petro na Yohana walikuwa hawana msaada na hawakuwa na elimu,lakini ukweli unabaki palepale kwamba walikuwa na Yesu na walitambua kwa vitendo kwamba jina la Yesu lina uweza kutenda maajabu. Walimuambia mtu katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri kusimama na kuondoka, na yule bwana akapokea uponyaji wake mara moja.

Kuna mtu anasoma ujumbe huu wakati huu, haijalishi umekosa msaada kiasi gani au umepoteza matumaini kiasi gani, hata kama ripoti ya madaktari ni mbaya kiasi gani, Bwana wangu, Yesu Kristo atabadilisha habari zako katika Jina la Yesu. Kupitia jina la Yesu magonjwa yasiyo na tiba yanatibika. Kupitia jina la Yesu, viwete watatembea na vipofu wataona. Kupitia Jina la Yesu wenye ukoma wanatakasika kimaajabu. Katika hii dunia yetu, ambapo magonjwa mapya yanaibuka kila sikuna yanawachanganya madaktari hata hawana ufumbuzi wakudumu au hata kuyatambua wanashindwa, unahitaji sana umtegemea huyu Daktari Mkuu – Bwana Yesu. Anao uwezo wa kuponya kila aliyevunjika moyo na kuharibu kila nguvu za kishetani. Kwa kuwa na Imani katika Jina lake na damu yake, uponyaj na ukombozi vinakuwa ni matukio ya kila siku.

watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya

Marko 16:18

“Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye”.

Yeremia 30:17

Kwa neema kuu ya Mungu, Yesu amekuwa daktari tangu nimekuja kufahamu kweli hii. Hii ndiyo sababu kila mara ninapopata nafasi ya kuwa hudumia watu, ninafuata tu maelekezo ya daktari wangu mwaminifu, na kumruhu ajitukuze mwenyewe. Sijawahi kuhangaika kwamba sijui uponyaji utatokeaje, mimi nanichofanya ni vile tu anavyoniamuru.

Moja ya chanzo kikubwa cha magonjwa ni dhambi. Kama unaishi maisha mabayo yanamfurahisha Mungu, magonjwa kamwe hayatapata nafasi mwilini mwako. Haijalishi watu wangapi wanapata magonjwakaribu na wewe, ahadi ya Mungu ya kuwaweka salama wana (watoto) wake dhidi ya magonjwa yanayowapata wengie iko palepale. Kama unaruhusu dhambi maishani mwako tambua kabisa kuwa utakuwa unatuma mwaliko kwa magonjwa kwa sababu dhambi na magonjwa vina uhusiano mkubwa. Tubu leo na ufuate njia ya uzima. Tunaporudi kwa Bwana, mataifa yetu pia yanaponyeka na jamii zetu pia zinaponyeka na hata magonjwa yanakuwa hayana nafasi kwao.

MAOMBI na wimbo wa kusikiliza kabla ya maombi

Chanzo cha Uzima (Anna Komba)
 1. Mtukuze Bwana kwa maneno ya kinywa chako au nyimbo.
 2. Mwambie Bwana naomba unisamehe dhambi zangu (Taja unazokumbuka)
 3. Baba, kwa jina la Yesu Kristo, naomba uniponye kila aina ya ugonjwa na maradhi.
 4. Baba, kwa Jina la Yesu, naomba unibatize kwa Roho Mtakatifu na moto wako ili kamwe nisikutane na magonjwa au maradhi tena.
 5. Baba, kuanzia leo ruhusu uponyaji wako uanze maishani mwangu.
 6. Baba, kwa Jina la Yesu naomba uwaguse ndugu zangu, marafiki (taja majina yao) na uwafanye wawe na afya njema.

NAMNA YA KUSOMA NENO LA MUNGU (BIBLIA / KITABU).

Ili uweze kusoma kitabu kwa ufasaha, unahitaji kushirikisha vidole vyako vyote vitano. Kwa namna hiyo hiyo ili uweze kulifahamu Neno la Mungu, vidole vitano vya mkono wako wa kulia vinahitajika sana. Hivyo vidole husimama badala ya kusikia, kusoma, kujifunza, kukumbuka na kutafakari juu ya Neno la Mungu.

 1. KUSIKIA (HEARING).

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”

WARUMI 10:17
 • Hii ni njia ya kujifunza Neno la Mungu ili upate uwezo wa kutenda mapenzi yake.
 • Unaweza kusilikiza Ujumbe, sauti, video, VCDs za watu walio na upako wa Mungu. Vinasaidia sana.
 • Lakini ufahamu wako kwa Mungu usiishie kusikia tu. Watu wa mambo ya elimu wanasema kuwa tunapokea asilimia 6 hadi 10 tu ya kile tunachokisia.
 • Mwamini ambaye ataishia kusikia tu ataweza kupata utapiamlo kwa kukosa mlo kamili hivyo atakuwa anateseka rohoni.
 1. KUSOMA (READING).

na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya

KUMBUKUMBU LA TORAT 17:19
 • Hii ni njia ya kumjua Mungu. Katika agano la kale kila mfalme aliyechaguliwa kuongoza watu alitakiwa asome Neno la Mungu kila siku.
 • Neno la Mungu ni chanzo cha nguvu. Ni kama ambavyo hizi nguvu za kawaida zinazalishwa na chakula, hivyo nguvu za kiroho zinazalishwa kwa kusoma Biblia. Wasomi wanasema tunashika asilimia 20 mpaka 25 ya tulichosoma.
 • Kuna Mwinjilisti wa Kimataifa anaitwa Dk. Billy Graham anashauri kusoma Zaburi tano, sura moja ya Mithali pamoja na sehemu nyingine za Biblia kwa siku.
 • Kwa kufanya hivi utaweza kusoma Zaburi na Mithali kila mwezi.
 • Zaburi inatusaidia kujenga Uhusiano wetu na Mungu, wakati Mithali inatusaidia kuboresha mahusiano mazuri na wanadamu wenzetu.
 1. KUJIFUNZA (STUDYING).

Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”

2 Timotheo 2:15
 • Kujifunza au kutafiti ni kutendea kazi kile tulichosikia au kusoma kwa kusudi la kuelewa, kuhifadhi na kutumia taarifa.
 • Tunahifadhi asilimia 50 tu ya tulichojifunza.
 • Kuna kina kirefu sana katika Neno la Mungu. Unaposoma ni kama tu kukwangua ardhi. Lakini jitahidi kujifunza ni kama vile unalima kuelekeza ndani ya hazina za siri.
 • Kujifunza kuna maanisha kuwa una chukua kila ufunuo mpya unaoupata unapokuwa umezama kusoma. Pia ina maanisha kujiuliza na kujijibu maswali wakati unasoma. Ina maanisha kulinganisha mstari mmoja na mwingine wa Biblia, na kutafuta mada na kujifunza yote ambayo unayaweza juu ya hiyo mada.
 • Kwa kadri unavyogundua kweli ndani ya Biblia, jali sana kuitendea kazi ile kweli, hapa unahitaji bidii ya kujaribu jaribu kila njia.
 1.  KUKUMBUKA (MEMORISING).

“Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”

ZABURI 119:11
 • Kukumbuka ni kutunza Neno la Mungu ndani ya akili yako kwa matumizi ya badaye.
 • Yaani unajisomea mstari wa Biblia kwa sauti. Unakariri neno kwa neno mpaka mstari mzima unakaa kwenye akili yako. Unaendelea kufanya hivi mpaka inafika mahali unakuwa ni Biblia inayotembea na Kuongea.
 • Kwa kufanya hivi unajikuta unabadilisha uwezo wako na maisha siku kwa siku.
 • Neno la Mungu ni silaha ambayo unaweza ukitumia kumpiga shetani katika kila gumu au hali ngumu. Mara nyingi sana unakutana na Mazingira ya vita na Biblia hauko nayo hapo.
 • Roho Mtakatifu atatumia Neno la Mungu ulilohifadhi ndani yako kuhakikisha unashinda mashamulizi ya adui au majaribu.
 • Neno la Mungu ni uhai. Kiwango cha Neno la Mungu kilichopo ndani yako kinaonesha kwa kiasi gani una uhai wa Mungu. Na kiwango cha uhai wa Mungu ndani yako kinaonesha Mungu wa kiasi gani umembeba ndani yako.
 • Neno la Mungu ndilo pekee linageuza nia au akili yako. Kutokana na kitabu cha Warumi 12:2. Kwa kuhifadhi Neno la Mungu ndani ya moyo wako, unaanza kufikiri Mawazo ya Mungu na kuona vitu kwa macho ya Mungu.
 1. KUTAFAKARI (MEDITATING).

“Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.”

Mwanzo 1:2
 • Kutafakari ni kulainisha Neno la Mungu. Ni ki kitendo cha kuhamisha Neno la Mungu kutoka Kichwani na kulileta moyoni, na kulifanya kuwa ndiyo sehemu ya kudumu ya maisha yako.
 • Wakati unasoma na kutafakari utaweza kubaini umekosea wapi, utaweza kubaini.
 • Mungu anakupa akili kupitia kutafakari ulichosoma na kushika kichwani.

Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”

Yoshua 1:8
 • Unapotafakari Neno linakupa umakini wa kuhakikisha unafanya ipasavyo.
 • Namna unavyowaza na Kuongea kutatawala maisha yako.
 • Hii ina maanisha hasa unachukua muda wa kuwaza juu ya mstari au aya, ukijiuliza maswali.
 • Akili yako lazima iwe wazi kusikia maongozi ya Roho Mtakatifu.
 • Hakikisha hamna kitu kinaingilia kile unawaza, na ukiwa katika hali hiyo Bwana atakupeleka kwenye safari ya ufunuo.
 • Kupitia kuwaza unaweza kupata siri za kufanikiwa, kuwa na amani ya milele, kustawi, na kila namna Mungu atakavyo.
 • Kusoma mavitabu mengi au makubwa hakubadilishi maisha yako, Yeye amesema tafakari Neno langu.
 • Hakuna kitu kiitwacho sijui maombi ya mpenyo (breakthrough), unachohitaji ni kujua na ustawi unakujia.

Faida za Kulijua Neno la Mungu:

 1. Neno linatupa kubadilika kutoka kushindwa hadi kushinda. Warumi 12:1-2
 2. Neno linatupa kujitambua na kuanza kutangaza kuwa mimi si maskini, si mgonjwa n.k
 3. Kuongeaa Biblia ni mwanzo wa kuliishi Neno la Mungu au ahadi za Mungu.

FOMU YA KUJIUNGA KWA AJILI YA USOMAJI WA BIBLIA KILA SIKU (WHATSAPP)

YUKO MLANGONI

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami

Ufunuo wa Yohana 3:20

Soma;

Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Ufunuo wa Yohana 3:19-22

Mungu ni wa Utaratibu, na Mbinguni ni mahali ambapo utaratibu upo. Kuna Itifaki ya hali ya juu sana mbinguni na mamlaka ambayo lazima iheshimike. Hivyo tunapo msogelea Mungu kuna namna ya kumwendea. Namna ya kuingia ndani ya nyumba au chumba inategemea kwamba utakaribishwa au utafukuzwa. Unatambua kuwa hata Mungu mwenyewe anajibana na kanuni ya utaratibu. Yesu alisema;

“Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”

Ufunuo wa Yohana 3:20

Ingawa Mungu alituumba, bado inamlazimu abishe hodi na anasubiri akaribishwe kabla hajaingia moyoni mwetu. Hata kama aliweka nafasi ndani ya moyo wako kwa ajili yake mwenyewe, na bado hatumii nguvu kuingia ndani ya moyo wetu. Ni jukumu lako kuamua kama aingie au asiingie kwako.

Ktika Mwanzo 18:1-8, tunaona Ibrahim aliona Wageni kutoka mbinguni karibu na hema lake. Alipowaona akawakimbilia, akawalaki na kuwandalia chakula waburudike. Alionesha wema wa hali ya juu sana kwao. Ukilitazama hili tukio utaona kuwa Mungu alisimama pembeni akisubiri wamkaribishe. Vilevile, katika Mwanzo 19:1-3 tunaona Lutu anawakaribisha malaika wawili katika Sodoma akawasihi sana waingie nyumbani kwake waweze kulala na kuoga.

Pia 2 Wafalme 4:8 Elisha alikuwa anapata njiani mwanamke mmoja wa Shunemu alimkaibisha nyumbani kwa chakula na alikuwa hata hana njaa, lakini yule mwanamke alimng’ang’ania aingie ndani. Baada ya hapo, ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula.

 1. Mungu anasubiri umkaribishe kwa sababu ya unyenyekevu wake. Na ni kwa sababu hataki kulazimisha kuingia ndani yetu.
 2. Alituumba sisi na uhuru wa kimaadili kama mawakili na si maroboti au mizimu.
 3. Anataka tuwe huwe huru kuonesha mapenzi yetu.
 4. Anataka tuwe huru kubeba mizigo ya matendo yetu ili tusije tukamtwisha lawama kwa matendo yetu wetu.
 5. Anataka kupima kama kweli tunampenda au la.

Kama bado hujaokoka, tambua kuwa unamtesa Mwokozi siku ulizoishi. Tafadhari itikia hodi yake kwenye mlango wa moyo wako. Tafadhari mkaribishe Yesu ndani, na ujisalimishe mzima mzima kwake. Kufanya hivi si amri ni maamuzi yako.

Chukua Hatua: Mkaribishe Yesu kwenye kila eneo la maisha yako ambayo ulimfungia nje.

Mtihani wa kidato cha sita umeahirishwa kutokana na janga la COVID-19 hadi hapo itakapoelezwa vinginevyo

Wizara ya elimu imesema mtihani wa kidato cha sita umeahirishwa hadi hapo itakapoelezwa vinginevyo kutokana na janga la #coronavirus.

Ratiba inaonesha kuwa mitihani ilikuwa ianze Mei 4 hadi Mei 21 mwaka huu. Wizara imewasihi wanafunzi kuendeleda kujisomea majumbani.

Wizara ya elimu nchini Tanzania imeahirisha mtihani wa kidato cha sita mwaka 2020 hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo kutokana na janga la virusi vya corona lililoikumba dunia.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Leonard Akwilapo wakati akijibu maswali kutoka kwa wazazi na wanafunzi wa kidato cha sita waliotaka kujua hatma yao baada ya Serikali kufunga shule zote.

“Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limesambaza barua kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya zote na katika shule za Umma na Binafsi kuwataarifu kuhusu kusitishwa kwa mitihani hiyo hadi serikali itakapotangaza vinginevyo,” amesema Akwilapo.

Kauli hiyo imekuja kufuatia wanafunzi na wazazi kuwa na maswali mengi endapo mitihani hiyo iliyopangwa kuanza Mei 04 mwaka huu, ingeanza kama ratiba inavyoonesha au la.

Licha ya mitihani kutokuwepo kama ilivyopangwa, wizara imewasihi wanafunzi kuendelea kujisomea muda wote wawapo majumbani.

Mapema Machi mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitangaza kufunga shule zote ikiwa ni miongoni mwa mikakati iliyochukuliwa na serikali kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona

Rai yangu: tukazane kuliombea taifa ili mambo yarudi katika Hali ya kawaida kama zamani.

KIJANA LINDA UBADAYE WAKO

“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.”

I Timotheo 4:12

“Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. 8 Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili. 9 Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. 10 Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.”

Mhubiri 11:7-10

Hali ya vijana kujiongoza wenyewe inaweza kuwa jambo hatari sana ikiwa itaachwa bila kusimamiwa. Inaweza hata kuacha alama isiyofaa kwa mtu mwenyewe kwa maisha yake yote. Je! Wewe bado ni kijana? Nina furaha wewe, lakini unahitaji kuzingatia kile Roho Mtakatifu anasema katika kitabu cha Mhubiri, kwa sababu katika ulimwengu wa leo ambapo mtandao hausahau, maadui wa umilele wako watawinda habari yoyote kuhusu makosa ya ujana wako wanapogundua uko njiani kwenda juu.

Maadui zako wasije wakapata chochote ambacho wanaweza kutumia kuharibu umilele wako katika Jina la Yesu. Katika uwanja wa kisiasa, wapinzani daima wanatafuta kile wanachoweza kutumia kuharibu hamu ya kisiasa ya kila mmoja. Vielelezo vingi vya jinsi wapiga kura wa kisiasa wanavyo tafuta hatua za zamani za wamiliki wa ofisi za kisiasa, wakiambia ulimwengu sababu nyingi ambazo hazipaswi kupiga kura kwa nguvu kulingana na mwenendo wa zamani, hata ukiweza kubadilika na kuwa bora. Kwa bahati mbaya, vijana wengi hawasikii ushauri wenye faida wakati wanafaa kutoka tabia moja mbaya kwenda nzuri wakati wa ujana wao.

Hadithi ya Reubeni katika Mwanzo 49: 3-4 inapaswa kuwa wito wa kuamka kwa kijana yeyote yule ambaye si mwadilifu anayesoma somo hili. Dhambi ambayo alifanya katika siku za nyuma, labda katika miaka ya mwisho ya miaka ishirini, ilileta shida kwa wakati ambao alipaswa kupokea baraka ya mzaliwa wa kwanza baadaye maishani. Labda alifikiri alikuwa mjanja, mzuri na hamu ya wanawake wote vijana, pamoja na mke wa baba yake, kiasi kwamba alilala naye (Mwanzo 35:22)! Jambo la kushangaza zaidi juu ya kesi hii ni kwamba Jakobo hakuwahi kutaja neno juu yake. Ikiwa angefanya hivyo, labda Rubeni angeliombea rehema. Mchungaji fulani aliharibu ushuhuda wao wa ndoa wakati bado walikuwa vijana kwa sababu haikuwahi kutokea kwao kuwaza kwamba watakuwa mchungaji baadaye maishani.

Kilichotokea, baada ya kuwa wachungaji, wanalazimika kuwa bubu wakati wowote majadiliano juu ya ukafiri wa ndoa yanapotokea. Hawawezi kutoa kihalali neno la ukweli juu ya jambo hili kwa sababu ya matendo yao ya zamani. Waalimu wengine wa Kikristo hawawezi kufichua kuwa wana watoto wangapi kwa sababu italeta swali kama “Je! Huyu kwa sasa ametulia kweli? Mama wa watoto hawa yuko wapi na kama hayupo, mama yao ni nani na yuko wapi? Alimuoa? Ikiwa ndio, ni vipi umeachana naye na kuwa mtu mwingine, kinyume na vile ambavyo umekuwa ukitufundisha sisi? Kuhusu ndoa.

DOKEZO : Kata marafiki ambao wanakuvuta kwenye vitu ambavyo vinaweza kusababisha kujuta baadaye katika maisha, na ujishughulishe na mshauri mkomavu, ambaye ni mfano wa kuigwa kwa kuisha maisha yampendezayo Kristo.