Mimi na wewe tu watumishi tunaotakiwa kufanya kazi kuu mbili kwa jinsi Mungu alivyotuumba. Jana nilifundisha kuwa Mtumishi ni yupi?

Utumishi wetu kwenye Mwili wa Kristo na utumishi wetu kwa kilichopotea.

UTUMISHI WAKO KWENYE MWILI WA KRISTO

Kwa kuongeza kuna mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu ambao Mungu amewatuma kuukamilisha watakatifu ili kuujenga Mwili wa Kristo. Kuna aina nyingi za utumishi:

Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya Imani. 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8  mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. 13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

Warumi 12:6-8, 13.

Kila mtu aliyezaliwa mara ya pili ndani ya familia ya Mungu amepewa nafasi au “utumishi” wa aina Fulani wa kutekeleza ndani ya Mwili wa Kristo. Ndani ya aya hiyo hapo juu tunaona aina nane za utumishi ambazo zimetajwa na tunapaswa kutekeleza kikamilifu na kila aina ya huduma ambazo Mungu hutupa kulingana na neema yake. Ametupatia:

Unabii, huduma ya vitendo, kufundisha, kushauri, kutoa, kusimamamia, kurehemu na utu wema.

UTUMISHI WAKO KWA ULIMWENGU

Tambua kuwa pia umewekwa hapo ulipo na upewa majukumu ili kuijaza dunia.

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe

Marko 16:15

Sisi sote tu wanafunzi wake. Na sote tumepewa kazi ya kuhubiri injili kwa kila kiumbe.

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Matendo ya Mitume 1:8

 Injili ya Ufalme wa Mungu lazima ihubiriwe ulimwenguni kote kwa ishara na ushahidi yaani maajabu, hapo ndipo mwisho utafika, ni sisi ndiyo tumeagizwa hiyo kazi – watu wa kawaida. Mungu anataka atuvuvie, atusheheneze na kutuwezesha na nguvu zake. Kuna maeneo matano ya kuhakikisha unayazingatia unapoanza kuhudumu kwa ulimwengu:

  1. Nimetumwa kwa nani?

Yesu alisema:

📖 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Luka 19:10

Hata mafarisayo walipomlaani Yesu kwa kula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, Yesu alijibu kwa kusema:

Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. 13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Mathayo 9:12-13

Tunaenda kuwatumikia wagonjwa, walio-wapweke, wanaoteseka, tunatakiwa kuwafikia wanaolia, waliopoteza matumaini na ambao hawana hata mtu wa kumgeukia.

  1. Ninaenda kutumikia nini?

Tunahitaji kujihoji, je tukifika kwa hawa tunaoenda kuwapa nini hasa? Je, nahitaji kuwapa chakula na mavazi hawa waliopotea au nahitaji kuwapa Neno la Mungu litakalo wafungua na kuwaweka huru?

Mara nyingi sana fursa ya kushuhudia inafunguka tunapotumika kwa kutoa vitu vya kimwili, acha sasa sisi tusiridhike kuhudumia kwa vitu tu bali tumtumikie mtu kamili (whole man). Hata Bwana Yesu alipokuja duniani aliharibu kazi za ibilisi, akaleta wokovu, aliponya wagonjwa, alifungua vipofu. Yeye ndiye mkate wa uzima na maji ya uhai.

📖 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Yohana 10:10

Wewe na mimi lazima tuhudumu kwa Neno la uzima na ukombozi, tuwape watu kweli ambayo itawaweka huru dhidi ya dhambi, tabia mbaya na magonjwa.

📖 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

Yohana 6:63

📖 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Yohana 8:32

Siyo tu kwamba utahudumu kwa Neno la uzima, lakini pia mimi na wewe lazima tuwe vyombo ambavyo nguvu ya uponyaji wa Mungu inapitia kuwaendea wengine. Lazima tutoe uthitishisho wa Neno!

Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Marko 16:17-18

  1. Ninaenda kutumika wapi?

Naomba nikuulize swali la msingi sana tena la kitoto lakini ni la muhimu sana. Samaki anapatikana wapi? Kwenye maji. Bata anapatikana wapi? Bwawani. Je, utawakuta wapi waovu? Wanaotafuta maisha, wenye njaa na waliopotea? Najua kuna mtu anawaza kuwa atawakuta nje ya milango ya majengo ya ibada wakisubiri kuingia. Kama kanuni ilivyo, huwezi kuwakuta watenda dhambi wakikaa kwenye mabenchi ya kanisani, utawakuta kazini, shuleni, kwenye mitaa yao, baa, kumbi za starehe kama disko, jela na kwenye nyumba za wenye heshima.

Yesu alisema mfano huu mkubwa:

📖 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.

Luka 14:23

  1. Nitaanzia wapi kutumika?

Je, kuna muda maalum ambao tunatakiwa kuanza kuwaendea waliopotea? Mara ngapi tumejikuta tumepoteza watu wengi kwa sababu hatukuwa tayari, ulihisi kuwa huwezi, hukuwa na utayari wa kutumia Imani. Katika kila mji kila siku kuna mtu anasubiri kulikia Neno la Mungu. Unaweza kuwa wewe ndiyo tumaini lao la mwisho ili waone pendo la Mungu na kuanza kuaishi kwa imani.

Leo ndiyo siku ya wokovu, tuko mbioni tunaukomboa wakati.

📖 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.

Yohana 9:4

Saa itakuja ambayo hakuna mtu ataweza kufanya kazi. Huu ndyo wakati wa kufanya kazi, usisubiri dakika moja mbele. Yesu anakuja hivi punde na unachotakiwa kufanya ni kutenda kazi zake sasa kwa kile uwezacho kufanya.

Huu ndiyo wakati ambao kila mwamini anatakiwa kutoa uthitibisho kuwa Yesu yu hai, anaponya, anakomboa, anafufua, anainua na anaweza yote. Huu ni wakati wa kuvuna roho za ulimwengu kwa Yesu.

  1. Nitahudumu namna gani?

Liko neno moja tu ambalo nataka ulijue kuwa ndiyo jibu la swali hili: NGUVU!

📖 Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

Yohana 6:28

Nguvu ya namna gani? Lazima tuingie tuzitenda kazi za Mungu kwa kudhihirisha nguvu ya Mungu atuleteayo Roho Mtakatifu. Kupitia nguvu tunaenda kuponya wagonjwa, kumfunga shetani, kuharibu kazi za ibilisi na kuwafanya vipofu waone.

Tunaenda kuthibitisha kwamba Yesu anaokoa, kwa watu mashuleni, kwenye ofisini, majumbani na kila Bwana atakapotuongoza.

Wazo kuu

Mungu anataka tukue kiufahamu wa Mungu na tuchukue nafasi zetu za haki ya kuwa wana wa Mungu anayeishi. Na tuzione nguvu zake zikithibitisha kila tutendalo maishani mwetu na tufanye mambo makubwa kuliko yoyote tuliyowahi kufanya hapo zamani. Mungu anakufunulia siri hizi ili akukabidhi nguvu yake, na utajua namna ya kutenda mambo katika nguvu ya Mungu na inawezekana usiitwe kuwa mtumishi wa madhabahuni, haijalishi wewe ni mfanyabiashara, mwanasheria, mwalimu, daktari, mama wa nyumbani – lakini utaweza kutoa uthibitho.

🗣 TUOMBE TENA KAMA JANA.

  1. Asante Baba Mungu kwa chakula hiki cha kiroho kilichonifikia.
  2. kwa jina la Yesu, ninaomba achilia upako wako – ili kila asomaye ujumbe huu ajitiishe kwako tangu sasa. Mpe ufahamu kwamba chapisho hili haliko mikoni mwake kwa bahati mbaya, bali ni kwa kusudi lako, hivyo ninaomba umtumie kwa utukufu na heshima yako.

Unaweza kujiunga kwenye group la PASTORBON WHATSAPP kwa kujaza fomu hapa chini: http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36

One thought on “MAJUKUMU YA WATUMISHI

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s