Ili uweze kusoma kitabu kwa ufasaha, unahitaji kushirikisha vidole vyako vyote vitano. Kwa namna hiyo hiyo ili uweze kulifahamu Neno la Mungu, vidole vitano vya mkono wako wa kulia vinahitajika sana. Hivyo vidole husimama badala ya kusikia, kusoma, kujifunza, kukumbuka na kutafakari juu ya Neno la Mungu.

 1. KUSIKIA (HEARING).

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”

WARUMI 10:17
 • Hii ni njia ya kujifunza Neno la Mungu ili upate uwezo wa kutenda mapenzi yake.
 • Unaweza kusilikiza Ujumbe, sauti, video, VCDs za watu walio na upako wa Mungu. Vinasaidia sana.
 • Lakini ufahamu wako kwa Mungu usiishie kusikia tu. Watu wa mambo ya elimu wanasema kuwa tunapokea asilimia 6 hadi 10 tu ya kile tunachokisia.
 • Mwamini ambaye ataishia kusikia tu ataweza kupata utapiamlo kwa kukosa mlo kamili hivyo atakuwa anateseka rohoni.
 1. KUSOMA (READING).

na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya

KUMBUKUMBU LA TORAT 17:19
 • Hii ni njia ya kumjua Mungu. Katika agano la kale kila mfalme aliyechaguliwa kuongoza watu alitakiwa asome Neno la Mungu kila siku.
 • Neno la Mungu ni chanzo cha nguvu. Ni kama ambavyo hizi nguvu za kawaida zinazalishwa na chakula, hivyo nguvu za kiroho zinazalishwa kwa kusoma Biblia. Wasomi wanasema tunashika asilimia 20 mpaka 25 ya tulichosoma.
 • Kuna Mwinjilisti wa Kimataifa anaitwa Dk. Billy Graham anashauri kusoma Zaburi tano, sura moja ya Mithali pamoja na sehemu nyingine za Biblia kwa siku.
 • Kwa kufanya hivi utaweza kusoma Zaburi na Mithali kila mwezi.
 • Zaburi inatusaidia kujenga Uhusiano wetu na Mungu, wakati Mithali inatusaidia kuboresha mahusiano mazuri na wanadamu wenzetu.
 1. KUJIFUNZA (STUDYING).

Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”

2 Timotheo 2:15
 • Kujifunza au kutafiti ni kutendea kazi kile tulichosikia au kusoma kwa kusudi la kuelewa, kuhifadhi na kutumia taarifa.
 • Tunahifadhi asilimia 50 tu ya tulichojifunza.
 • Kuna kina kirefu sana katika Neno la Mungu. Unaposoma ni kama tu kukwangua ardhi. Lakini jitahidi kujifunza ni kama vile unalima kuelekeza ndani ya hazina za siri.
 • Kujifunza kuna maanisha kuwa una chukua kila ufunuo mpya unaoupata unapokuwa umezama kusoma. Pia ina maanisha kujiuliza na kujijibu maswali wakati unasoma. Ina maanisha kulinganisha mstari mmoja na mwingine wa Biblia, na kutafuta mada na kujifunza yote ambayo unayaweza juu ya hiyo mada.
 • Kwa kadri unavyogundua kweli ndani ya Biblia, jali sana kuitendea kazi ile kweli, hapa unahitaji bidii ya kujaribu jaribu kila njia.
 1.  KUKUMBUKA (MEMORISING).

“Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”

ZABURI 119:11
 • Kukumbuka ni kutunza Neno la Mungu ndani ya akili yako kwa matumizi ya badaye.
 • Yaani unajisomea mstari wa Biblia kwa sauti. Unakariri neno kwa neno mpaka mstari mzima unakaa kwenye akili yako. Unaendelea kufanya hivi mpaka inafika mahali unakuwa ni Biblia inayotembea na Kuongea.
 • Kwa kufanya hivi unajikuta unabadilisha uwezo wako na maisha siku kwa siku.
 • Neno la Mungu ni silaha ambayo unaweza ukitumia kumpiga shetani katika kila gumu au hali ngumu. Mara nyingi sana unakutana na Mazingira ya vita na Biblia hauko nayo hapo.
 • Roho Mtakatifu atatumia Neno la Mungu ulilohifadhi ndani yako kuhakikisha unashinda mashamulizi ya adui au majaribu.
 • Neno la Mungu ni uhai. Kiwango cha Neno la Mungu kilichopo ndani yako kinaonesha kwa kiasi gani una uhai wa Mungu. Na kiwango cha uhai wa Mungu ndani yako kinaonesha Mungu wa kiasi gani umembeba ndani yako.
 • Neno la Mungu ndilo pekee linageuza nia au akili yako. Kutokana na kitabu cha Warumi 12:2. Kwa kuhifadhi Neno la Mungu ndani ya moyo wako, unaanza kufikiri Mawazo ya Mungu na kuona vitu kwa macho ya Mungu.
 1. KUTAFAKARI (MEDITATING).

“Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.”

Mwanzo 1:2
 • Kutafakari ni kulainisha Neno la Mungu. Ni ki kitendo cha kuhamisha Neno la Mungu kutoka Kichwani na kulileta moyoni, na kulifanya kuwa ndiyo sehemu ya kudumu ya maisha yako.
 • Wakati unasoma na kutafakari utaweza kubaini umekosea wapi, utaweza kubaini.
 • Mungu anakupa akili kupitia kutafakari ulichosoma na kushika kichwani.

Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”

Yoshua 1:8
 • Unapotafakari Neno linakupa umakini wa kuhakikisha unafanya ipasavyo.
 • Namna unavyowaza na Kuongea kutatawala maisha yako.
 • Hii ina maanisha hasa unachukua muda wa kuwaza juu ya mstari au aya, ukijiuliza maswali.
 • Akili yako lazima iwe wazi kusikia maongozi ya Roho Mtakatifu.
 • Hakikisha hamna kitu kinaingilia kile unawaza, na ukiwa katika hali hiyo Bwana atakupeleka kwenye safari ya ufunuo.
 • Kupitia kuwaza unaweza kupata siri za kufanikiwa, kuwa na amani ya milele, kustawi, na kila namna Mungu atakavyo.
 • Kusoma mavitabu mengi au makubwa hakubadilishi maisha yako, Yeye amesema tafakari Neno langu.
 • Hakuna kitu kiitwacho sijui maombi ya mpenyo (breakthrough), unachohitaji ni kujua na ustawi unakujia.

Faida za Kulijua Neno la Mungu:

 1. Neno linatupa kubadilika kutoka kushindwa hadi kushinda. Warumi 12:1-2
 2. Neno linatupa kujitambua na kuanza kutangaza kuwa mimi si maskini, si mgonjwa n.k
 3. Kuongeaa Biblia ni mwanzo wa kuliishi Neno la Mungu au ahadi za Mungu.

FOMU YA KUJIUNGA KWA AJILI YA USOMAJI WA BIBLIA KILA SIKU (WHATSAPP)

One thought on “NAMNA YA KUSOMA NENO LA MUNGU (BIBLIA / KITABU).

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s