MAJUKUMU YA WATUMISHI

Mimi na wewe tu watumishi tunaotakiwa kufanya kazi kuu mbili kwa jinsi Mungu alivyotuumba. Jana nilifundisha kuwa Mtumishi ni yupi?

Utumishi wetu kwenye Mwili wa Kristo na utumishi wetu kwa kilichopotea.

UTUMISHI WAKO KWENYE MWILI WA KRISTO

Kwa kuongeza kuna mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu ambao Mungu amewatuma kuukamilisha watakatifu ili kuujenga Mwili wa Kristo. Kuna aina nyingi za utumishi:

Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya Imani. 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8  mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. 13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

Warumi 12:6-8, 13.

Kila mtu aliyezaliwa mara ya pili ndani ya familia ya Mungu amepewa nafasi au “utumishi” wa aina Fulani wa kutekeleza ndani ya Mwili wa Kristo. Ndani ya aya hiyo hapo juu tunaona aina nane za utumishi ambazo zimetajwa na tunapaswa kutekeleza kikamilifu na kila aina ya huduma ambazo Mungu hutupa kulingana na neema yake. Ametupatia:

Unabii, huduma ya vitendo, kufundisha, kushauri, kutoa, kusimamamia, kurehemu na utu wema.

UTUMISHI WAKO KWA ULIMWENGU

Tambua kuwa pia umewekwa hapo ulipo na upewa majukumu ili kuijaza dunia.

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe

Marko 16:15

Sisi sote tu wanafunzi wake. Na sote tumepewa kazi ya kuhubiri injili kwa kila kiumbe.

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Matendo ya Mitume 1:8

 Injili ya Ufalme wa Mungu lazima ihubiriwe ulimwenguni kote kwa ishara na ushahidi yaani maajabu, hapo ndipo mwisho utafika, ni sisi ndiyo tumeagizwa hiyo kazi – watu wa kawaida. Mungu anataka atuvuvie, atusheheneze na kutuwezesha na nguvu zake. Kuna maeneo matano ya kuhakikisha unayazingatia unapoanza kuhudumu kwa ulimwengu:

 1. Nimetumwa kwa nani?

Yesu alisema:

📖 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Luka 19:10

Hata mafarisayo walipomlaani Yesu kwa kula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, Yesu alijibu kwa kusema:

Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. 13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Mathayo 9:12-13

Tunaenda kuwatumikia wagonjwa, walio-wapweke, wanaoteseka, tunatakiwa kuwafikia wanaolia, waliopoteza matumaini na ambao hawana hata mtu wa kumgeukia.

 1. Ninaenda kutumikia nini?

Tunahitaji kujihoji, je tukifika kwa hawa tunaoenda kuwapa nini hasa? Je, nahitaji kuwapa chakula na mavazi hawa waliopotea au nahitaji kuwapa Neno la Mungu litakalo wafungua na kuwaweka huru?

Mara nyingi sana fursa ya kushuhudia inafunguka tunapotumika kwa kutoa vitu vya kimwili, acha sasa sisi tusiridhike kuhudumia kwa vitu tu bali tumtumikie mtu kamili (whole man). Hata Bwana Yesu alipokuja duniani aliharibu kazi za ibilisi, akaleta wokovu, aliponya wagonjwa, alifungua vipofu. Yeye ndiye mkate wa uzima na maji ya uhai.

📖 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Yohana 10:10

Wewe na mimi lazima tuhudumu kwa Neno la uzima na ukombozi, tuwape watu kweli ambayo itawaweka huru dhidi ya dhambi, tabia mbaya na magonjwa.

📖 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

Yohana 6:63

📖 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Yohana 8:32

Siyo tu kwamba utahudumu kwa Neno la uzima, lakini pia mimi na wewe lazima tuwe vyombo ambavyo nguvu ya uponyaji wa Mungu inapitia kuwaendea wengine. Lazima tutoe uthitishisho wa Neno!

Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Marko 16:17-18

 1. Ninaenda kutumika wapi?

Naomba nikuulize swali la msingi sana tena la kitoto lakini ni la muhimu sana. Samaki anapatikana wapi? Kwenye maji. Bata anapatikana wapi? Bwawani. Je, utawakuta wapi waovu? Wanaotafuta maisha, wenye njaa na waliopotea? Najua kuna mtu anawaza kuwa atawakuta nje ya milango ya majengo ya ibada wakisubiri kuingia. Kama kanuni ilivyo, huwezi kuwakuta watenda dhambi wakikaa kwenye mabenchi ya kanisani, utawakuta kazini, shuleni, kwenye mitaa yao, baa, kumbi za starehe kama disko, jela na kwenye nyumba za wenye heshima.

Yesu alisema mfano huu mkubwa:

📖 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.

Luka 14:23

 1. Nitaanzia wapi kutumika?

Je, kuna muda maalum ambao tunatakiwa kuanza kuwaendea waliopotea? Mara ngapi tumejikuta tumepoteza watu wengi kwa sababu hatukuwa tayari, ulihisi kuwa huwezi, hukuwa na utayari wa kutumia Imani. Katika kila mji kila siku kuna mtu anasubiri kulikia Neno la Mungu. Unaweza kuwa wewe ndiyo tumaini lao la mwisho ili waone pendo la Mungu na kuanza kuaishi kwa imani.

Leo ndiyo siku ya wokovu, tuko mbioni tunaukomboa wakati.

📖 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.

Yohana 9:4

Saa itakuja ambayo hakuna mtu ataweza kufanya kazi. Huu ndyo wakati wa kufanya kazi, usisubiri dakika moja mbele. Yesu anakuja hivi punde na unachotakiwa kufanya ni kutenda kazi zake sasa kwa kile uwezacho kufanya.

Huu ndiyo wakati ambao kila mwamini anatakiwa kutoa uthitibisho kuwa Yesu yu hai, anaponya, anakomboa, anafufua, anainua na anaweza yote. Huu ni wakati wa kuvuna roho za ulimwengu kwa Yesu.

 1. Nitahudumu namna gani?

Liko neno moja tu ambalo nataka ulijue kuwa ndiyo jibu la swali hili: NGUVU!

📖 Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

Yohana 6:28

Nguvu ya namna gani? Lazima tuingie tuzitenda kazi za Mungu kwa kudhihirisha nguvu ya Mungu atuleteayo Roho Mtakatifu. Kupitia nguvu tunaenda kuponya wagonjwa, kumfunga shetani, kuharibu kazi za ibilisi na kuwafanya vipofu waone.

Tunaenda kuthibitisha kwamba Yesu anaokoa, kwa watu mashuleni, kwenye ofisini, majumbani na kila Bwana atakapotuongoza.

Wazo kuu

Mungu anataka tukue kiufahamu wa Mungu na tuchukue nafasi zetu za haki ya kuwa wana wa Mungu anayeishi. Na tuzione nguvu zake zikithibitisha kila tutendalo maishani mwetu na tufanye mambo makubwa kuliko yoyote tuliyowahi kufanya hapo zamani. Mungu anakufunulia siri hizi ili akukabidhi nguvu yake, na utajua namna ya kutenda mambo katika nguvu ya Mungu na inawezekana usiitwe kuwa mtumishi wa madhabahuni, haijalishi wewe ni mfanyabiashara, mwanasheria, mwalimu, daktari, mama wa nyumbani – lakini utaweza kutoa uthibitho.

🗣 TUOMBE TENA KAMA JANA.

 1. Asante Baba Mungu kwa chakula hiki cha kiroho kilichonifikia.
 2. kwa jina la Yesu, ninaomba achilia upako wako – ili kila asomaye ujumbe huu ajitiishe kwako tangu sasa. Mpe ufahamu kwamba chapisho hili haliko mikoni mwake kwa bahati mbaya, bali ni kwa kusudi lako, hivyo ninaomba umtumie kwa utukufu na heshima yako.

Unaweza kujiunga kwenye group la PASTORBON WHATSAPP kwa kujaza fomu hapa chini: http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36

MTUMISHI NI YUPI?

Uko njiani kuelekea mpenyo wa kiroho katika maisha yako ambao utakupeleka mbali sana zaidi ya matarajio yako uliyowahi kujiwekea. Nakuhakikishia kwamba kwa kadri utakavyozidi kusoma na kuongeza kweli hizi ndani ya roho yako, mstari kwa mstari na amri kwa amri, hutakuwa kama ulivyokuwa. Maisha yako yatabadilishwa, utapokea upako mpya wa nguvu za Mungu. Utajua namna ya kuzitenda kazi za Mungu!

Lengo kubwa la masomo haya ni kukufanya uweze kutoka katika hali ya mazoea na kuingia katika hatua ya viwango vipya, kuwa mpya kabisa na chombo chenye ufanisi mara mia. Yaani utakuwa ni mtumishi ambaye Mungu na watu wanajivunia uwepo wako maana utakuwa mwanajeshi ambaye unawafugua watu kutoka kwenye vifungo na utumwa wa adui katili, shetani. Na hii ndiyo kazi ya Mungu.

Katika mfululizo wa fundisho hili kwa yeyote atakaye zingatia sana jiandae kuingia kiwango kikubwa ambacho hujawahi kufikiria kufikia na hujawawahi kuwa nacho. Mungu tunayemtumikia ni Mungu ambaye hana mipaka, tunahitaji kufikia kiwango cha kuwa na nguvu za Mungu ambapo hatutazuiliwa na chochote.

UMEITWA ILI KUTUMIKA

Mikononi mwako kuna kazi za badaye za Mungu. Huduma ya kufanya kazi za Mungu si ya madhabahuni tu, maana wengi wanajiona hawahusiki tunapozungumzia huduma. Siku za leo, neno mtumishi tunalielewa kama ni la watu ambao wameenda shule za Biblia au seminari. Lakini tafsiri ya neno mtumishi kwa Kigriki ni kutumika. Yesu alilisitiza sana umuhimu wa kuwa watumishi. Tunaliona hili katika aya ifuatayo ambapo maneno yote mawili yametumika:

📖 “Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; 28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”.

Mathayo 20:26-28

Maana halisi ya neno “mtumishi” linakuja kupatikana hapa. Yesu alisisitiza sana umuhimu uvumilivu wa kweli kwa mtu ambaye kweli anataka kutumika. Kwa maneno mengine niseme kwamba, kabla hujawa mtumishi lazima uwe tayari kujitoa (kwa kutoa muda wako, kipaji chako, fedha zako na chochote ulichonacho)kama Yesu alivyojitoa kama fidia ya wengi.

Sisi sote, uwe daktari, mwanasheria, mhasibu, mke wa nyumbani, mjane na kila mtu anayesema Yesu ni Bwana anaweza kuwa mtumishi kwenye maana ya neno na “kuzitenda kazi za Mungu”.

Wazo kuu

Ni kwamba kila mshirika wa kanisa la kwanza alikuwa mtumishi. Mtume Paulo alimuagiza Timotheo kuwashirikisha wengine kweli aliyoiona na kusikia.

📖 Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.

2 Timotheo 2:2

Inaonesha kuwa kila mtu katika kanisa la Kwanza alikuwa mtumishi japo sio wote walihubiri kama Petro na Paulo ingawa walikuwa ni watumishi. Neno la Mungu likaenea nyumba kwa nyumba. Hatuwezi kuufikia ulimwengu wote kwa kile kiitwacho eti utumishi wa madhabahuni tu, kila mshirika wa Mwili wa Kristo ni Mtumishi. Ni kweli huduma tano zilikuwepo katika kanisa la kwanza, lakini zilitenda kazi sawa na mpango wa Mungu. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwakamilisha watakatifu ili waweze kutenda kazi ya huduma! Na kila mtu akawamtumishi.

Wanawake waliosafiri pamoja na Bwana Yesu na wanafunzi walifanya kazi ya kupika chakula, lakini pia ndiyo walikuwa wa kwanza kubeba habari za kufufuka kwa Bwana Yesu kuwapelekea wanafunzi. Dorkasi alitumika kupanda mbegu na kugawa nguo kwa wahitaji. Stephano alikuwa mmoja wa watu saba waliochaguliwa kwenda kulikuza kanisa na akadhihirisha ishara na miujiza kwa watu wake.

📖 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

Waefeso 4:11-12 “

Mungu anataka akutumie kwa namna yako

Mungu anataka uwe mwakililishi wake, ukitoa uthibitisho wa kwamba Yesu yu hai. Giza la dhambi limetawala mazingira yakuzungukayo na anataka wewe uweze kuangaza kama nuru. Ametoa nafasi ambayo wewe pekee unaweza kuijaza. Wenye dhambi wanatakiwa waone wewe unavyowamulikia na wakufuate toka mbali. Mungu hataki watakatifu waondoke duniani (Zaburi 16:3). Anataka watumishi wote kwa kazi zao waweze kuangaza nuru wanapofanyia kazi.

📖 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Mathayo 5:14:-16

Mimi na wewe tunao wajibu wa aina moja, na kwa wajibu huu Bwana Yesu ametupatia nguvu na uwezo ambao unatufanya tuwe washindi na kuangaza kama nuru katika dunia hii, tukiwaleta waume kwa wake kwa Kristo. Mimi na wewe tu watumishi tunaotakwa kufanya kazi kuu mbili. (Somo litaendelea kesho)

🗣 TUOMBE

 1. Asante Baba Mungu kwa chakula hiki cha kiroho kilichonifikia.
 2. kwa jina la Yesu, ninaomba achilia upako wako – ili kila asomaye ujumbe huu ajitiishe kwako tangu sasa. Mpe ufahamu kwamba chapisho hili haliko mikoni mwake kwa bahati mbaya, bali ni kwa kusudi lako, hivyo ninaomba umtumie kwa utukufu na heshima yako.

Unaweza kujiunga kwenye group la PASTORBON kwa kujaza fomu hapa chini: http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36

WATOA UTHIBITISHO -II

TUFANYAJE KUZITENDA KAZI ZA MUNGU?

📖 Yohana 6:28 Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

Mungu anaendelea kuongea na watumishi wake kama alivyoongea na akina Ibrahimu, Henoko, Musa, Eliya, Isaya na wengineo wengi. Bado anaongea na watu wake kama zamani, na ujumbe huu ni maongezi yake kwetu. Katika sura ya 18 ya kitabu cha Mwanzo tunaona Mungu alipanga kuiangamiza Sodoma na Gomora kutokana na maovu yao, lakini ili atimize hilo, tunasoma swali la ufunuo:

📖 Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo? Mwanzo 18:17

Bwana alitaka kumshirikisha mtumishi wake. Bwana aliongea na mtumishi wake na akamwambia mipango yake. Na katika mstari wa 19 anafunua siri kwa nini aliamua kuongea na Ibrahimu. Alisema:

📖 Kwa maana nimemjua …

Mungu alimjua Ibrahimu kuwa atafanya kwa kipau mbele jambo ambalo Bwana atamwambia. Bwana alijua kuwa Ibarahimu atamwamini huyu mtu na ataweza kuongea naye kibinadamu. Yakobo anatuambia kwamba Ibrahimu aliitwa “rafiki wa Mungu” (Yakoo 2:23)

Musa pia alikuwa rafiki wa Mungu ambaye waliweza kuongea ana kwa ana na kumfunulia mipango yake:

📖 Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake … Kutoka 33:11

📖 Amosi 3:7 inasema “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.”

Ahadi hizi siyo tu za kipindi cha zamani, maana Mungu tuliye naye ni Mungu ambaye kamwe habadiliki, yupo nyakati zote na habadiliki. Mungu hajaacha kuongea na watu wake katika mambo yake. Anataka kujifunua kwetu mara zote, lakini anajifunua kwa watu waaminifu kama alivyokuwa anajifunua kwao zamani.

Mwaka 2004 nilihudhuria mkutano wa kiroho katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, uliongozwa na Mwalimu Christopher Mwakasege, kwa mara ya kwanza nilisikia sauti ikiongea nami kama wazo kuwa “jiandae ukikua utafanya kazi hii, utaenda mataifa mengi kwa ajili yangu”. Haikupita nusu saa nikamsikia Mwalimu pale madhabahuni akisema kuna watoto wako hapa Bwana anataka niwaombee kwa kazi ya injili siku zijazo, tukapita mbele akaomba kuna maneno aliniambia nilimshangaa sana Mungu. Mwaka 2006 nilifunga siku tatu na kwa mara ya kwanza tulikuwa mlimani nikiomba na rafiki yangu Gasper Mungu akaongea nami tena, na hapo alinionyesha jinsi ambavyo atawaadhibu watendao dhambi – siwezi kusahau hadi leo. Toka kipindi hicho nilianza kujitambua kuwa mimi nitakuwa mtumishi wa Mungu!

Mwaka 2012 ndipo alipoongea nami tena waziwazi, nikiwa nasali kanisa langu lilelile la KKKT, akaniambia sasa nataka uanze kujifunza namna ya kunitumikia na nitakupeleka mahali pa kukua kiroho kwa haraka, nikapewa kuchagua mtumishi wa kunilea mmoja yuko Nigeria na mwingine yuko Tanzania. Katika ndoto hiyo niliambiwa changua nani akulee kati ya hao – sikujibu chochote, ndipo nikafunga na baada ya mfungo wa siku tatu nikajikuta jumapili ya disemba 16, 2012 nikiwa njiani kwenda kanisani (Lutheran), likaja wazo kwa nguvu sana kwamba tafuta kanisa la Efatha hapa Songea, sikujua kama pana kanisa la Efatha Songea, nilipowauliza watu wakaniambia lipo Mkuzo, hata mtaa wa Mkuzo pia sikuwahi kuusikia. Nikapanda daladala na nikafanikiwa kufika hapo na ndipo nikamkuta mmoja wa wale niliombiwa nichague anilee – Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na akaongoza ibada na nikawa na amani tele ya kuokoka siku hiyo. Na kweli nikaokoka kwa kuongozwa na yeye mwenyewe, baada ya ibada akaniambia ukimaliza chuo kikuu unifuate Mwenge, na hata sasa ndiye aliyeniingiza rasmi kwenye utumishi huu wa kichungaji. Siku moja Bwana Yesu aliniambia usendelee kuhangaika kutafuta wa kumuoa bali mke ambaye utamuoa ni Vaileth, na siku nyingine akanitokea waziwazi na kusema fundisha viongozi wako (Julai 24, 2014). Sitaeleza yote hapa!

Wazo kuu

Mungu bado anaongea na watu wake hata leo, anasema kwa njia nyingi ikiwemo; Neno lake, muziki, watu, matukio yanayojirudia, mazingira, ndoto, maono, Roho Mtakatifu, mawazo, sauti ya wazi, amani na ishara namiujiza isiyo ya kawaida. Mungu daima anatuongoza, anatuelekeza, anatuonya, anatutia moyo, anatuahidi, anatufurahisha, tunatakiwa kuwa makini na kuuijua sauti yake ili tusiwe viziwi wa kiroho. Tutaweza kuzitenda kazi zake endapo tu tutafanya bidii kuisikia sauti yake hata kama dunia imejaa mashaka na mitazamo mingi.

Hatua za kusikia sauti ya Mungu

 1. Tuliza akili yako.
 2. Mfanye Mungu kuwa Mshauri wako namba moja.
 3. Uwe makini.
 4. Imarisha uhusiano wako na Mungu.
 5. Soma Biblia yako
 6. Fanya ibada (abudu)
 7. Daima tulia na kusikiliza

Je, unazifahamu njia nyingine ambazo Mungu anatumia kuongea na watu? Ziweke kwenye comment hapa chini.

🗣 TUOMBE

 1. Ee Baba, nisaidie kujua njia zako kwa namna nyepesi, niweze kukutumikia na kuuleta ulimwengu kwa Yesu Kristo!

Unaweza kujiunga kwenye group la PASTORBON la WhatsAPP kwa kujaza fomu hapa chini: https://forms.gle/957djapjw8gFLkF36

Pia, Like page ya Facebook: https://fb.me/boniemwa

WATOA UTHIBITISHO

SISI TU WATOA UTHIBITISHO

Matendo ya Mitume 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Roho Mtakatifu anakuja juu ya maisha yetu kwa kusudi. Ametolewa na Bwana Yesu kwetu waamini kwa ajili ya ulimwengu. Ubatizo wa Roho Mtakatifu sio kwa ajili ajifurahisisha kwetu au kubarikiwa tu. Kuna wajibu ambao tunapaswa kuutekeleza kulinana na vipawa vya Roho Mtakatifu ulivyopewa.

Kazi za Mungu zinafanywa kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu pekee.

Yesu analiweka sawa hili anaposema tutapokea nguvu, au uwezesho, Roho Mtakatifu atakapotujilia juu yetu. Ukweli hasa hili ni kwamba nguvu itatufanya kuwa watoa uthibitisho wa Neno la Mungu kwa watu wa mataifa (wasio-okoka) kwamba Yesu yu hai. Tumeitwa tumeteuliwa na kuwezeshwa kama mashahidi rasmi wa Bwana Yesu kupitia uwezesho wa Roho Mtakatifu.

Wazo kuu

Yesu kupitia kwa Roho Mtakatifu, ametoa ahadi ya kukuwezesha na kukupa uwezo usio wa kawaida ili uweze kutoa uthibitisho kwamba Yu hai. Na hili ndilo kusudi kubwa la Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Uwezo wote wa kiungu, uwezo usio wa kawaida wa Roho Mtakatifu umeachiliwa kwetu ili tuweze kufanya kazi ya ushahidi.

📖 Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”.

Hatua za uanafunzi.

Kuna hatua tatu za msingi ambazo zinatimizwa ndani yako pale Roho  Mtakatifu anapokuwezesha uweze kuwa mtoa uthibitisho wa kwamba Yesu yu hai. Kwanza, anakupa uwezo wa kunena Neno la kweli lenye nguvu kwa kuhubiri injili kwenye maisha ya watu. Pili, anangára maishani mwako kupitia uwepo wake ili Kristo aonekane kupitia wewe. Tatu, Roho Mtakatifu anakupatia vipawa vya mawasiliano kupitia ishara, miujiza na maajabu. Haya ni maisha ya kweli, ambayo Mungu anataka ukue katika hayo kama mwanafunzi wa Kristo.

Soma: Matendo 1:4-8

🗣 TUOMBE

 1. Asante Roho Mtakatifu kwa matendo yako ya ajabu ndani yangu, na kwa kunisaidia niweze kutenda mambo makuu, katika Jina la Yesu, Amina.
 2. Ee Bwana, napokea uwezo wako wa kiungu ili kuuthibithishia ulimwengu kwamba uko hai na ni Bwana wa wote. Nijaze kwa upya leo kwa ajili ya kazi inayoendela. Ruhusu dunia ikuone WEewe ndani yangu ttangu sasa, katika Jina la Yesu nimeomba.

Unaweza kujiunga kwenye group la PASTORBON WhatsApp kwa kujaza fomu hapa chini: http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36

NITAKUREJESHEA AFYA YAKO

Sikiliza live ya somo hili HAPA

Jamii kubwa ya wanadamu inateseka sana na magonjwa na kila aina ya mateso. Ashukukuriwe Mungu kwa neema yake ya uponyaji nimeeleza Jana Bwana atakurudishia afya. Ni mapenzi mapenzi ya Mungu ya dhati Sana kuona watu wake Wana afya njema. Yesu alibeba maumivu yetu yote ili sisi tuishi maisha ya uhuru dhidi ya dhambi na maradhi. Yesu tabibu mkuu hapendi kupoza mgonjwa. Nikuombe siku ya leo sahau mapito yako, maana kuna watu wanaamini hawawezi kuponywa kwa sababu dhambi zao za nyuma bado zinakumbukwa mbele yao.

“Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.”

Kutoka 23:25
 1. Utumishi wako

Bwana wetu anataka kuona tunamtumikia Yeye daima na hili lipo tangu uumbaji, alimweka Adam na Hawa ili wamtumikie Yeye. Huku dunianikuna watu wameamua kumtumikia ibilisi, kuna wengine hawajaamua kumtumikia ibilisi lakini Bwana hawamtumikii, hivyo hawaeleweki wanamtumikia Bwana au ibilisi, hii ni hatarisana.

 1. Baraka zinatoka kwake

Matokeo ya kumtumikia Bwana ni kwamba chakula unachokula kinabarikiwa na maji unywapo pia yanabarikiwa. Kwa kuwa vimebarikiwa na Bwana vinafanyikawa tiba dhidi ya kila sumu na magonjwa ndani ya mwili wako. Tazama maajabu ya chakula cha mfalme Nebukadreza walikula mtama na maji tu, lakini kwa sababu waliamua kusimama upande wa Bwana akakibarikia chakula chao mara zote na tazama Biblia inasema;

“Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme”. Danieli 1:15

 1. Uponyaji wake unakujilia.

Ikiwa umeamua kuwa mtumishi wa Mungu, ukampa moyo wako wote na macho yako yakapendezwa na njia au sharia ya Bwana (Zaburi 119:140, Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda). Unafika mahali unagundua hakuna kitu kizuri na kitamu kama ahadi zake.

Bwana akishaona umefika hali pa kulipenda Neno lake na kuishi kwa kumtegemea Yeye ndipo anaamua kukufungua vifungo vyako dhidi ya kila mateso. Ndiyo maana amesema;

Zaburi 107:17-20 “Wapumbavu, kwa sababu ya ukosaji wao, Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa. 18 Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti. 19 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. 20 Hulituma Neno Lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao”.

Mathayo 8:8, 13 “Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. 13 Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile”

Luka 5:17 “Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya

Mungu wetu anatuma Neno ili kuponya, na leo acha nikufikishie ujumbe wake kwako wewe msomaji.

NINI KIFANYIKE ILI ATUME UPONYAJI?

Mathayo 9:12-13 “12 Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. 13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Mungu wetu haponyi matajiri tu, anaponya wote na

KWA NINI UOMBE?

Yeremia 33:3-6 “Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. 4 Maana Bwana, Mungu wa Israeli asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu, na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga; 5 Wanakuja kupigana na Wakaldayo, lakini ni kuzijaza kwa mizoga ya watu, niliowaua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, ambao kwa ajili ya uovu wao wote nimeuficha mji huu uso wangu. 6 Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli”.

MAOMBI

Kumbukumbu 32:39 “Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu”

 1. Baba, tunakushukuru kwa kutupa neema ya funuliwa siri zako wakati huu.
 2. Baba, kwa jina la Yesu tunaomba rehema kwako kwa dhambi zetu na kila aina ya uovu.
 3. Ee Baba, naomba uniponye dhidi ya ugonjwa wa (taja jina), ponya nafsi yangu

Karibu WhatsApp Group kwa mafundisho zaidi kwa kujaza fomu hii: https://forms.gle/957djapjw8gFLkF36