KANUNI KUMI ZA NDOA BORA

Zifuatazo ni kanuni 10 za ndoa bora.

1. KANUNI YA NENO LA KUPENDEZA

Usipitishe siku nzima bila kutamka neno la kupendeza na la kukumbukwa na mwenzio kwa muda wote ambao hautakuwepo. Soma Mithali 17:22 na Mithali 10:1

2. KANUNI YA NENO “NIMEFURAHI KUKUONA”

Usikutane na mwenzio bila kumkaribisha kwa kauli ya upendo. Soma Mwanzo 18:2-3 na Mwanzo 19:16-20

3. KANUNI YA KUTAWALA HASIRA

Usiwe mwepesi wa kukasirika. Soma Mithali 14: 17-18, Mithali 16:32, Yakobo 1:19.

4. KANUNI YA KUDHIBITI ULIMI.

Usiongee kwa sauti kubwa na mwenzako. Soma, Mithali 10:32, Mithali 17:28 na Mithali 19:29

5. KANUNI YA UWAJIBIKAJI

Usiruhusu mwenzio arudie kuuliza swali. Soma, Mithali 12:4, 26.

6. KANUNI YA UKARIMU

Usifanye Jambo kwa gharama za wengine. Mithali 3: 27-28.

7. KANUNI YA UTII

Wapenzi wawili mko sawa. Ni mameneja wawili ambao kila mmoja ana majukumu yake ndani ya taasisi moja iitwayo ndoa. Soma, Mwanzo 3:16-19.

8. KANUNI YA KUZIKA MAKOSA

Usifufue makosa, labda kama yanajirudia mara kwa mara. Siku zote ongea kwa upendo kuhusu hilo. Mithali 21:16

9. KANUNI YA USAFI WA JAMBO

Siri ya furaha iko kwenye kusahau yaliyopita na kuanza kila siku na mambo safi. Soma, Mithali 17:1

10 KANUNI YA MUUNGANO WA THAMANI

Muda wote ukiwa na nafasi kaa na mwenzi wako. Soma Mwanzo 2:24.

INALIPA

MOYO WA KIONGOZI – IV

Kiongozi Bora anahitajika Sana katika jamii ya leo. Watu wanatamani mtu ambaye atawaongoza awe na sifa ya ubora katika utendaji wa uongozi wake. Watu wanataka moyo wa kiongozi ambao unamheshimu Mungu kuliko wao anavyojiheshimu yeye. Kiongozi ambaye anapenda kujitunza, kujua na kujitoa sadaka kwa faida ya wengine.

Moyo wa kiongozi ni wa muhimu kuliko umbile au sura yake.

Tazama, kwa mfano Manisha ya Yusufu. Habari zake tunazisoma katika kitabu Cha Mwanzon 35-50. Ni habari inayoshangaza ya utawala na neema ya Mungu. Katika watu waliotajwa agano la kale Yusufu ni mmoja kati ya kiongozi mwenye viwango vya ubora wa juu, hakuwa na dhambi kwa sababu alikuwa ana hofu ya Mungu.

Nataka kusema hivi,

natamani moyo wa Yusufu uwe ndo mwakilishi wa kila kiongozi bora, na kila kiongozi atamani kuwa nao.


Moyo wa kiongozi daima una fikra chanya zitokanazo na ndoto yake.

Yusufu alikuwa muota ndoto. Zile ndoto zake zikamsababishia matatizo kadhaa, lakini aliweza kuona kile ambacho wengine hawakioni. Aliona picha kubwa ya ubadaye wake. Ukweli hii picha ilitoka kwa Mungu, na nina amini kwamba Mungu ametupa sote uwezo wa kuota. Kiongozi yeyote mzuri lazima awe na maono yanayompa kuvumilia magumu, kuvumilia kuonewa, kuvumilia watu anaowaongoza, yanayompa umuhimu was kusamehe na kusonga mbele.

Mch. Boniface Evarist

WhatsApp (+255752122744).