Somo lote linapatikana katika 2 Mambo ya Nyakati 20:1-30

2 Nyakati 20:1-5: Mataifa matatu yaliunda umoja wa kumvamia Yehoshafati kivita. Biblia inaweka wazi kuwa Yehoshafati akaogopa. Kwa sababu hii wakakusanyika ili wamtafute BWANA kutoka miji yote ya Yuda walifunga na kuomba. Ilibidi liitishwe Kusanyiko kuu haraka ili wamtafute BWANA, Nyumbani mwa BWANA.

HATUA SABA ZA UKOMBOZI WA KWELI.
1. Tambua mamlaka ya Mungu.
2Nyakati 20:6”akasema, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.”

Yehoshafati hakuomba kitu hapa cha kwanza alimtambua yule aliye msaada wake. Alitambua anamuomba Muumbaji wa mbingu na vitu. Maombi yasiyo ya kawaida yalimjia mfalme kwa sababu ya ufahamu wake kwa Mungu na ile hofu ndo ikaleta ibada kwa mfalme. Alichokifanya ni kusema BWANA kabla sijaomba chochote nataka ujue kuwa Natambua wewe una uweza na nguvu ya kufanya chochote.

2. Tambua Ahadi zake.
2Nyakati 20:7 “Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele? 7 Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele? 8 Nao walikaa humo, wamekujengea patakatifu pa jina lako humo, wakisema 9 Yakitujia mabaya, upanga, hukumu, au tauni, au njaa, tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako, (maana jina lako limo katika nyumba hii), na kukulilia katika shida yetu, nawe utasikia na kuokoa.”

Neno la Mungu leo kwa kila hitaji tulilo nalo tunamwendea Mungu kwa Ahadi zake. Sasa ndipo unasema baba ulisema utasikia shida zetu na kutuokoa. Na unamwambia uliagana na baba zetu (Kiblia Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kwa wewe wakati huu ni Josephat, Philipo na Mimi Boniface), wewe ni mtawala, na ulitupa ardhi hii tuimiliki. Na hapa pia unatakiwa useme kile wewe umefanya kwa ajili ya Mungu mfano. Kumjengea Bwana hekalu.

3. Tambua Msaada wako.
2Nyakati 20:12 “Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yatazama kwako. 13 Wakasimama Yuda wote mbele za Bwana, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.”

Maana msaada wako hautoki kwa mtu au vitu. Unafika wakati katika kila uhitaji tulio nao maishani mwetu unahitaji kumwamini Mungu. Hatukutegemea hii vita na hatujajipanga, tunaomba uingilie kati Mungu. Jambo lolote unahitaji msaada wa Bwana. Kuwa shirika na familia, waamini wenzio katika kusanyiko.

4. Tambua vita si yako ni Mungu
2Nyakati 20:14”Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya Bwana, katikati ya kusanyiko;15 akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu.”

Unapofikia hatua ya kutambua msaada ulipo. Mungu anainua nabii wa kukuambia njia ya namna ya kushinda. Katika yote unayopitia Mungu anaenda kufanya jambo ambalo hajawahi kukutendea. Jambo la msingi kulingalia ni wewe kuweka hofu mbali nawe “usiogope”. Alitoa Ahadi kuwa nitakuponya, nitakupa mahitaji, nitakupigania, nitakulisha. Acha hofu! Mtukuze Bwana maana katika lolote una ushindi wa asilimia mia moja. Si wewe ulitoa Ahadi, Mungu ndiye aliyetoa Ahadi.

Vita kamwe haijawahi kuwa kati yako na shetani toka mwanzo. Tangu shetani alipojiinua na kupigwa vita haijawahi kuwa yako. Kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziharibu kazi za ibilisi (1 Petro 3:8). Vita ni ya BWANA!

5. Acha vyote na uanze kusifu na kumwabudu Mungu.
2Nyakati 20:17“…Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi. Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana.19 Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana”

Hii inafanana sana na kauli ya Musa aliyowaambia wana wa Israeli katika Bahari ya Shamu. (Kutoka 14:13)

Sikiliza nikuambie mwana wa Mungu, chakula cha Mungu ni pale unapomsifu na kumwabudu. Hakuna kitu Mungu anafurahia kama kumsifu na Kumwabudu. Acha kulialia katika yote unayopita nayo hakikisha unamsifu Mungu utashangaa huelewi namna gani ugonjwa, au maadui na kila tatizo vinatoweka mbele zako.

Biblia inasema “21 Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. 22 Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa.”

6. Mwamini mungu na Mtumishi wake.
2Nyakati 20:20“Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.”

Mwaminini Mungu katika Neno au Ahadi zake, Usithubutu kujenga hofu kwake. Na Mtumishi wake akisema jua wazi kuwa hilo ndilo litakalokuwa. Usisite maana hii ni kanuni ya rohoni! Maana Mungu hata Fanya jambo lolote duniani bila kuwafunulia manabii wake (Amosi 3:7).

7. Chukua mateka kwa shukrani, usibweteke .
Soma: 2 Nyakati 20:25-30.
Chukua mali zote ulizonyang’anywa na wabaya wako, fedha, afya, kazi, mashamba, biashara, n.k. vyote teka kwa jina la Yesu.
Hakuna vita itakushinda endapo utaelewa haya mambo saba na ukayatekeleza katika maisha yako. Haleluya!
——————————————-

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s