Ni Kwa Ajili Ya Mema Yako

Tangu mwanzo, namna ambavyo shetani anafanya kazi amekuwa akipanda mbegu ya mashaka katika mioyo wa watu ambao Mungu amewawekea mpango maalum na kusudi la Mungu kwao. Mfano, wakati lengo la Mungu kumkataza Adam na Eva wasile tunda lililokatazwa lilikuwa ni kuwafanya waishi milele, wenye afya na ustawi, shetani akawaendea na kuwaambia eti Mungu kawakataza kwa sababu hawataki mema (Mwanzo 3:4-5).

Ni aina hii ya mashaka ambayo shetani alipanda kwa ndugu zake Yusufu baada ya kifo cha baba yao. Ashukuriwe Mungu Yusufu alikuwa mtu anajua Mawazo ya Mungu; akawazima mashaka yao mara moja. Kwa sisi wana wa Mungu siku hizi, Mungu ametufunulia mpango wake na makusudio yake kwetu katika Yeremia 29:11:

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”

Hili si wazo jipya kwa Mungu, isipokuwa hili limekuwa kusudio la Mungu kwengu tangu mwanzo wa uumbaji (Mwanzo 1:26). Elewa kuwa ni dhambi kuwa na mashaka dhidi ya mema katika nia ya Mungu. Anapotuongoza kufanya jambo au kuishi kwa namna fulani ambayo ni kinyume na namna ambayo shetani au watu wanatutegemea sisi kuishi kwayo.

Kwa kuwa Yusufu alifahamu Mawazo ya Mungu kuhusiana na yote yaliyomtokea alikataa kufanya ibada ya mashujaa kutoka kwa ndugu zake na akatuliza mashaka yao. Aliwafariji kwa kuwafanya waelewe kuwa matendo mabaya waliyomfanyia yalitokana na Mungu ili akamilishe kusudi lake katika maisha ya Yusufu.

Mwanzo 50:19-20 “Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? 20 Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.”

Kwa lugha nyingine Yusufu alikuwa anawaambia ndugu zake kuwa haikuwa wao ila Mungu aliyemtuma yeye Misri kwa kusudi lililo wazi sana. Ndiyo maana Mtume Paulo akasema;

Warumi 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”

Bwana anasema na wewe kuwa acha kulalamika Kuhusu nini kinatokea kwako leo; ni kwa ajili ya mema yako. Mambo yako yatakuja kuwa mazuri sana endapo utaendelea kumpenda Mungu hata kama utakuwa katika hali mbaya sana, ambayo ina kusudi la kiungu. Narudia tena kukuambia wewe: ni kwa ajili ya mema yako, na muda si mrefu utajua ni kwa nini.

Mwanzo 50:15-21 “Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. 16 Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema, 17 Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye. 18 Nduguze wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako. 19 Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? 20 Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. 21 Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.”

Omba: Baba, kutokana na Neno lako, mambo yote yafanyike mema kwa kusudi lako juu yangu, katika Jina la Yesu.

Dhamiri Ya Wazi Isiyo na Hatia

Matendo ya Mitume 24:16 “Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.”

Kanisa la Kristo duniani litakuwa na afya sana endapo wakristo wote watakuwa na dhamiri ya wazi ya kuogopa kufanya makosa. Cha ajabu ni kwamba mara kwa mara makosa mengi sana yanajitokeza katika mwili wa Kristo. Hii inatokana na kutumia vibaya fursa tupatazo, utajiri na vitu tunavyo miliki.

Ili kupanda mema kanisani ni lazima tufuate kanuni za kiroho ambazo Mtume Paulo alituwekea katika 1 Timotheo 6:17-18:

Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. 18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;”

Namba kubwa ya Wakristo bado wanaishi chini ya kifungo cha dhamiri iliyo jaa hatia. Kwa nini? Ni kwa sababu hawajaamua kuachana na ukale wao kabla wa wokovu. Mfano, utakuta mtu kaokoka lakini bado anaishi na mwanamke ambaye si mke wake wa kwanza. Wengine bado wanaishi kwenye nyumba ambazo walijenga kwa fedha za uizi au dhuruma. Wengine wanaona ni kazi kuzuia mahusiano yao na makundi au marafiki wenye vikao vya kishetani.

Hayo na matatizo mengine mengi ni vikwazo vinavyosababisha watu kupata uhuru kamili. Baadhi ya watu wa namna hii huwaweka wachungaji wao kwenye kibano, kwa sababu matatizo yao yanagoma kuondoka. Hivyo huonesha kuwa pengine Mchungaji hana upako wa kutosha kukabiliana na matatizo yao. Hivyo utakuta wana hama kanisa mara kwa mara ili kupata kanisa ambalo atapata raha dhidi ya matatizo yake, lakini bado hawapati raha ya roho zao.

Matumizi mabaya ya mali na nafasi, hasahasa yale yaliyo mali au nafasi vilivyopatikana kinyume cha sheria, hukwamisha sana uhuru wa dhamiri. Ndiyo maana maisha ya amani, furaha na ridhaa yaliyotegemewa, ambayo ndiyo tegemeo letu kubwa tunapo okoka na yanayotufanya kuwa wa kipekee kama wana wa Mungu, yametuepuka kwa hila.

Kuna msemo usemwao sana na Wakristo wanaoshutumiwa kwa matumizi mabaya ya mali na nafasi zao usemao “Dhamiri yangu hainihukumu mimi.” Swali ni: dhamiri ipi hiyo unayoiongelea? Ni ile ya wafu waliokataliwa? Baadhi yao hudiriki hata kusema “Wale wote waongozwao na Roho, hao ndiyo wana wa Mungu.” Roho gani unayoingelea? Inaweza kuwa roho ya Mungu, ambayo iliyovuvua uandishi wa Neno la Mungu na ikageuka leo kuwa kile roho wa Mungu aliwaoongoza watu kuandika ilikuwa ni makosa?

Mpendwa tusijidanganye wenyewe zaidi ya hapo. Tuamue kuishi maisha ya Kikristo, maisha yanayo tutoa kunako hatia dhidi ya Mungu na watu, na hasahasa wale watu wa nyumbani katika imani.

Warumi 14:16-21 “Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya. 17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu. 19 Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. 20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza. 21 Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.”

Omba: Baba kwa Damu ya Yesu, niondolee makosa na dhamiri mbaya ya kazi zangu zote zilizokufa ambazo huniletea hatia, katika Jina la Yesu.

Upendo wako Uko Wapi?

Wakolosai 3:2 “Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.”

Nimebaini kuwa wakiristo wengi wanashindwa kuishi maisha ya viwango vya maagizo ya Biblia kwa sababu wanapenda sana vitu vya duniani kuliko vya mbinguni, na sababu ya hili ni kutokana na kuja kwa kupenda utajiri wa mali kama kanisa. Naweza kuwa je ni makosa kuwa tajiri? Hapana! Ibrahim alibarikiwa sana, Isaka alibalikiwa sana na Yakobo pia alibarikiwa sana. Na bado hawa wote walimtumikia Bwana. Mfalme Daudi alimbariki BWANA kwa ustawi wa vitu pamoja na vingine vingine.

Zaburi 103:1&5 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;”

Hivyo napenda kusema neema unayohitaji ili kutawala utajiri wa vitu ni kubwa kuliko ile ya kutawala umaskini. Mungu anapoanza kukubariki lazima uzidi kuomba kwa bidii sana ili kutawala ustawi wako kinyume na hapo mapenzi au upendo wako utahama toka vitu vya mbinguni na utapenda vya dunianiani sana.

Ni upumbavu wa hali ya juu sana kumpenda na kumtumikia Mungu wakati u maskini wa vitu vya duniani, unakuta mtu anamsahau Mungu akipata mali aliye mpa nguvu za kupata utajiri. Ndiyo maana Biblia inasema;

MITHALI 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.”

Wana wa Mungu wengi sana wakati wana hangaika kupata kipato walisema “Baba ufalme wako uje” lakini baada ya kufanikiwa wanaishi maisha kama vile hawatakufa kamwe, na kama vile Yesu hata kuja wakati wowote. Si kazi ngumu kabisa kuwabaini watu ambao upendo wao uko kwa vitu vya mbinguni, kwa sababu saa zote utawaona wako na kazi ya kujenga na kuupanua ufalme wa Mungu. Kwa sababu uwekezaji wao ni wa Mbinguni, na mioyo yao muda wote inawaza juu wa mbinguni.

MATHAYO 6:20-21 “bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; 21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

Hakuna uhakika wa hazina unayoitunza na kuweka duniani. Uwekezaji wako katika vitu vya mbinguni ndicho utakachobaki nacho baada ya kuingia mbinguni. Hivyo basi, anza kuweka matamanio juu ya vitu vya mbinguni tangu sasa.

Soma: Wakolosai 3:1-6 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. 5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”

Omba: Mpenzi Roho Mtakatifu, jaza moyo wangu na upendo kwa ajili ya vitu vya mbinguni katika Jina la Yesu.

KUWAJALI MASKINI

Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.” – KUMBUKUMBU LA TORATI 15:11

Biblia inazungumza jambo moja muhimu sana juu ya wito wetu kama wanafunzi wa Yesu, ambapo wengi wetu hatujali sana hilo. Jambo lenyewe linahusiana na kuwajali maskini.

Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake.” – MITHALI 22:9

Moja ya njia ya haraka sana ya kubarikiwa na Mungu ni kuwasaidia maskini. Mungu mwenye nguvu Amesema maskini hawataisha kamwe huku duniani, na ni haki yake kuwajali maskini. Lazima tuelewe kuwa Mungu hata kuja duniani kufanya jambo hili wakati sisi wanadamu tupo. Ameshatoa amri kwa walio na kipato au mali kuwapa wale wasio na kipato. Hivyo yeyete anayewajali sana maskini kwa kuwasaidia atabalikiwa sana na Mungu wetu. Hii ni moja ya siri za baraka za Kiungu.

Mbali na baraka za hapa duniani kwa wale wanaowahudumia maskini, Bwana wetu Yesu Kristo anaenda mbali zaidi na kutuhakikishia baraka za uzima wa milele. Alisema watu wa namna hii watazawadiwa thawabu ya kutosha katika ufalme wa Mungu.

Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;” – MATHAYO 25:34-35.

Niliwahi kusoma habari za kiongozi mmoja mkubwa sana wa dini pale Nigeria ambaye alitoa ushuhuda wa namna alivyookoka wakati nchi yao wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kutokana na maelezo yake huyo mtu alikuwa ana kimbia kimbia yale machafuko akajikuta kambilia kwa wanandoa fulani wa Kikristo na hao wanandoa walimpokea nyumbani kwao. Alishangaa sana kuona ndani ya muda mfupi mama mwenye nyumba akaleta sahani kubwa ya wali na kuweka mbele yake. Alisahangaa sana namna gani kaandaa chakula cha kutosha kiasi kile na namna gani waliweza kutoa chakula kizuri kama kile kwa mkimbizi kama yeye.

Baada ya muda naye akaamua kuungana na familia ile kumtumikia Mungu ambaye aliitunza familia iliyomwokoa wakati wa vita. Kwa jinsi ya kusaidiwa tu ndiyo ukawa mwanzo wa yeye kubadili dini na kuwa Mkristo. Leo, hii amefanikiwa sana katika huduma ambayo Mungu amempa imeenea dunia nzima Makanisa yake.

Hapa Ukweli ni kwamba wale waliompokea na kumuongoza katika njia ya wokovu wanafaidi matunda ya kuokoa roho za watu pamoja naye na mbinguni wanasubiri cheo chao.

Omba: Baba, nipe neema ya kutoa misaada, nataka kuwajali na kuwatunza maskini katika Jina la Yesu Kristo.

HATUA YA KUGEUKA IV

MHUBIRI 5:10 “Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba maongeo. Hayo pia ni ubatili.”

Gehazi alikuwa ni mtumwa wa nabii Elisha. Alipewa nafasi ya kuwa mwanafunzi wa nabii mkubwa na alikuwa na nafasi ya kurithi ule upako wa mara mbili wa nabii Elia uliokuwa juu ya Elisha. Ingawa tamaa zake ziliikimbiza hatma yake ya kuwa nabii mkubwa sana hapo badaye. Aliamua kumtafuta vitu vya kila siku vya dunia hii kwa gharama ya wito wa kinabii alioupata. Alikuwa na mtazamo wa vitu vya kidunia sana na hata akaapa mbele za Mungu kuwa lazima “amiliki vitu / mali”. Kama wahubiri wa siku hizi, ni kama alisema “… anayefanya kazi madhabahuni lazima ale vya madhabahuni” zingatia maneno yake 2 Wafalme 2:20

“Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake.”

Baada ya dhambi yake ya tamaa kujulikana na bwana wake, ukoma wa Naamani ukahamia kwake na vizazi vyote baada ya yeye (2 Wafalme 5:27)

Yuda Iskarioti ni mfano wa mtu mwingine ambaye tunapaswa kujifunza kwake. Alikuwa na maadili na matatizo ya kiroho kama vile Gehazi; tamaa na mlafi. Biblia inasema kwamba alikuwa mwizi, na licha ya kuwa Mhasibu wa Huduma ya Yesu mara nyingi aliiba katika mfuko wa fedha (Yohana 12:4-6). Ulafi wake ulimfikisha hatua ya maamuzi yaliyo mpelekea hatia ya Kukosa uzima wa milele; aliamua kumuuza Bwana wake, mfalme wa Utukufu (Mathayo 26:14-16). Kabla Yuda Iskariote hajatambua ujinga wake, alijipotezea nafasi ya kuhesabika miongoni mwa Mitume kumi na mbili. Aliishia kujinyonga.

Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. 5 Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.” Mathayo 27:3&5.

Wana wa Mungu katika nyakati hizi lazima wawe na hofu na vitu vya kidunia. Vinaua, Ingawa huwezi kugundua haraka. Ndiyo maana Yohana mpenzi wa Yesu alituonya walimwengu kama vile alijua kanisa litakavyokuwa siku za mwisho (1 Johana 2:15-17.

Omba: Baba, niongoze kamwe nisije nikafanya maamuzi ambayo yataweka giza katika ubadaye wangu katika Jina la Yesu. Amen.