YOHANA 15:2 “Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.”

Maneno”mkazae matunda” yalianza katika Mwanzo 1:28, pale ni kama agizo, lakini pia tunaweza ita ni baraka. Na tunajua Neno la Mungu ni lazima litimie, halirudi bure.

Yohana 15:8 “Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.”

  1. Baba anatukuzwa sana tunavyozaa sana.
  2. Tunaonesha kuwa wanafunzi wake.

Na mtu asiyezaa matunda Mungu humhesabu kama ni muasi wa agizo la kusudi la uumbaji wake.

Mathayo 21:19 “Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.”

Mtini huu na mfano wa Talanta Mathayo 25:14-30 unaonesha wazi kuwa Mungu Anataka kutuona sisi tukizaa matunda. Pia mifano hii inaonesha wazi kuwa Mungu atahukumu kwa kigezo cha kuzaa matunda, kwa kiasi cha matunda yenyewe na ubora wake.

Mungu anategemea sisi tuzae matunda kwa katika maeneo kama

1. Kuvuna roho za watu.

2. Utakatifu

3. Haki

4. Upendo na

5. Fedha

Ni muda mzuri kujitathimini je wewe unazaa matunda? Kwa wale wanaozaa matunda ni muda mzuri wa kuzaa zaidi. Ukibaini kwamba wewe huzai matunda Mungu anakupa nafasi ya pili, tumia nafasi hii kuzaa matunda kwa uaminifu sana. Ili uweze kuzaa matunda yakupasa uwe na;

1. Wokovu halisi (confessing your sins and giving life to Jesus lets deliverance)

2. Ukae ndani ya Mungu (Total submission to the will of God). Hapa unapata neema ya kuwa mzaaji matunda.

Soma: Luka 13:6-9 “Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. 7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? 8 Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; 9 nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.”

Maombi:

1. Bwana naomba usimkate huyu asikiaye fundisho hili wala usimbadirishe katika nafasi yake kwa Jina lenye uweza la Yesu Kristo.

Chukua hatua: Mwambie “Baba, nipe kuzaa matunda katika kila eneo la maisha yangu, kwa Jina la Yesu ninaomba”

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s