Anza Jambo Jipya Dogo Tu

AYUBU 8:7 “Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.”

Mwanzo wa jambo ni wa muhimu sana kwa sababu unasasidia kuwa kama msingi ambapo kila kitu kinasimama. Namna unavyoanza jambo linaonesha ile spidi, tabia na kiwango cha kufaulu ama kufeli utakacho pambana nacho katika jambo au mradi huo. Nina habari njema wako: kwamba kama Yesu yuko upande wako, daima unaweza kuanza upya jambo, hata kama umepoteza matumaini kiasi gani.

Hakuna kupoteza matumaini kwake atembeaye na Mungu. Yeye ni nguvu na chanzo cha kila kitu unachotaka kuvipata katika maisha yako (Wakolosai 1:17). Katika hali yoyote ambayo umepoteza matumaini ya kushinda baada ya kushindwa mara nyingi, ukimshirikisha Yesu utaweza kuanza mwanzo mpya. Petro alikuwa amekata tamaa anaosha nyavu zake ili akapumzike lakini Bwana Yesu alipofika (Luka 5:2-6).

Kibinadamu Petro alifanya kila alichopaswa kufanya. Alifika mtoni mapema sana Asubuhi, alikuwa na vifaa vya kufanyia kazi na alienda na timu nzuri ya wasaidizi, bado hakupata majibu mpaka Alfa na Omega alipofika. Yesu atakujia katika kila eneo unalo hangaika nalo katika Jina la Yesu.

Moja ya changamoto kubwa ya wanao mwamini Yesu ni kukosa uwezo wa kumpatanisha majira ya Mungu na yao. Tunapata ugumu wa namna ya kuunganisha maisha yetu ya sasa na ubadaye wetu. Tunatakiwa kuelewa kuwa Mungu amejikita katika Kusababisha vitu visivyo na thamani kuvipa heshima. Mungu anaweza kukuita wewe ni Meneja wakati unafanya kazi kama mtumwa, anaweza kukuita wewe ni bilionea wakati hata hujui utatoa wapi chakula cha muda mchache ujao. Tatizo kubwa la Wakristo ni Kukosa imani na hofu kile Mungu kawaitia. Wengi wamebakia katika hali ileile kwa kitambo kirefu kwa sababu tu wana hofu kuanza kwa imani. Wengi wamepoteza fursa nyingi sana kwa sababu tu hawako tayari kuacha starehe zao. Milango mingi mikubwa imefungwa kwa sababu wale ambao ilifunguliwa kwao hawana ujasiri wa kutenda. Eti, kwa sababu umejaribu kila njia ili ufanikiwe na hujafanikiwa na hujafanikiwa basi ndiyo umekataa tamaa.

Unachotakiwa kufanya ni kumwita Alfa ambaye ni Yesu. Atakupa mwanzo mpya kabisa, na atakuongoza mpaka ule mwanzo wako mdogo unageuka kuwa mkubwa sana. Kamwe usidharau siku za mwanzo mdogo. Huwezi kupata utukufu bila historia. Hakikisha kwamba kila wakati unamtukuza Mungu kwa kila hali unayopita nayo kimaisha. Watu wengi sana wanachanganyikiwa na kile kikubwa Mungu anafanya na wengine maisha ya wengine, wakiacha kusherehekea kidogo ambacho Mungu hutenda kwao.

Kamwe usiidharau biashara inayoanza kidogo. Kamwe usiidharau nafasi yako ya kazini inayoanza kama haina maana. Kamwe usidharau Mazingira ambayo hayaoneshi matumaini ya ushindi. Kamwe usidharau ndoa inayo anza kwa udogo. Kiwango ulicho nacho sasa si chako, uko katika hatua ya kufikia uendako na haiwezekani ukawa hivyo mpaka dunia ione utukufu wa Mungu katika maisha yako.

Soma:

Zakaria 4:8-10 “Tena neno la Bwana likanijia, kusema,9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu.10 Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.

Daima Ubarikiwe Msomaji,

Mch. Boniface Evarist.