Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”

Kuna silaha mbili zivutiazo ambazo zipo kwa wana wa Mungu katika vita vya kiroho. Nazo ni Neno [la Mungu] na Damu [ya Yesu]. Neno ana nguvu sana kiasi kwamba dunia nzima iliumbwa na Yeye (Yohana 1:1-3). Hii ndiyo sababu Neno lina uwezo wa kukuondolea kila jambo linalotatanisha maisha yako na kuwa sawasawa, kama alivyofanya katika Mwanzo 1. Kifo ni tatizo kubwa sana ambalo linapambana na mwanadamu. Lakini Biblia inatufunulia siri kwamba nguvu ya mauti ipo kwenye dhambi:

“Uchungu wa mauti ni dhambi.” – 1 Wakorintho 15:56a

Lakini ashukuriwe Mungu kwamba Damu ya Yesu alichukua nguvu ya dhambi mara moja na kwa wote. Ufunuo 1:5b inasema kuwa:

Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,”

Pale dhambi inapo shughulikiwa na Damu isiyo na hatia ya Yesu Kristo. Uchungu wa mauti unakosa nguvu.

Kwa sababu hiyo mwana wa Mungu akivaa hizi silaha mbili yaani Neno na Damu, ushindi umeamuliwa kwake. Swali ni hili: kwa nini Baadhi ya wana wa Mungu wanaishi maisha ya kushindwa? Tatizo ni kwamba ili hizi silaha mbili za vita vya kiroho zifanye kazi kwake, masharti fulani lazima yatekelezwe. Moja ya masharti hayo ni kwamba lazima wawe tayari kuliheshimu Neno la Mungu, Haijalishi gharama yake ni kubwa kiasi gani. Wakati mwingine wana wa Mungu wakikamatwa katika dhambi za kutisha ambazo hata hazitakiwi kusika kwa waadilifu, wana kimbilia kusema “ni kazi ya shetani”. Ni kama vili kwenye Biblia zao Yohana 10:10 wamefutiwa. Kwa sababu Wakristo wa aina hii hawa heshima Neno la Mungu kwa kulitunza, maana Neno hafanyi kazi kwao. Endapo mwana wa Mungu anaendelea kumkisi mwanamke mwingine tofauti na mke wake ni wazi kwamba analipuuzia Neno la Mungu. Imeandikwa

jitengeni na ubaya wa kila namna.” -1 Wathesalonike 5:22.

Neno halitaweza kuwa na nguvu kwake katika kupambana na watu kama Delila. Pia Damu ya Yesu Kristo ambayo ailimwagika kwa kutobolewa na misumari kwenye mikono yake bila namba isiyo hesabika ya kugonga na kutoa haitakuwa kitu kwao. Zingatia sana Neno hili la umaliziaji katika Ufunuo wa Yohana 12:11 linasema hivi:

ambao hawakupenda maisha yao hata kufa

Ili Damu ya Yesu ifanye kazi kwako, unatakiwa kuikataa dhambi kwa kiwango hiki ikiwezekana cha kumwaga damu yako mwenyewe (Waebrania 12:4 anasema: Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi).

Ninakuombea kwamba Neno na Damu atatenda miujiza kwako mara zote katika Jina la Yesu.

Waebrania 12:22-25 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, 23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, 24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. 25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana

CHUKUA HATUA: Amua kuweka Neno la Mungu katika matumizi sahihi kwenye maisha ya kila siku na isihi Damu ya Yesu Kristo dhidi ya kila Mazingira mabaya kwa ajili ya kuweza kutenda mazuri tu.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s