Umewahi kuwa na hofu ya kuomba msaada wakati unahitaji msaada zaidi? Je, umewahi kuwa katika hali ngumu sana kusita na kufikiria mara mbili mbili juu ya kuomba usaidiwe kwa kitu fulani? Nina hakika sote katika baadhi ya nyakati tuliona aibu kuuliza, lakini naweza kuwahakikishia, si aibu au hofu. Najua wengi wetu wanataka kufanya mambo juu yetu wenyewe na kwa uhuru wao bila ya msaada wa watu wengine, na wengi wetu tunaongoza maisha bila msaada kutoka kwa watu wengine, lakini kamwe usiogope kuuliza wakati unahitaji kusaidiwa, kwa sababu najua kuna mambo hatari ambayo yanaweza kutokea kwa mtu kama hataki kuomba msaada.

Hivyo mambo mengi yanaweza kutokea, ebu filikia mtu fulani akanyanyua kitu kizito na haombi msaada, ni lazima mgongo kuanza kuuma au au kupata maumivu makali sana. Usione aibu kuomba msaada, wakati unaogopa kuomba msaada watu ghafla, wanaanza kuteta ama kukuwazia kama wewe unajiona kuwa shujaa, yaani unatumia kila njia kuuonesha umma kwa bidii na  kuvutia watu kwa kufanya kila kitu mwenyewe, lakini si kufanya hivyo tutaleta picha nzuri. Hapo unadhuru mwili wako na afya yako kwa kufanya hivyo.

Daima ni vema kufikiri kabla ya kutenda jambo kwa sababu wakati msaada upo na wakati huohuo kuna watu wanakuuliza kama unataka msaada juu ya jambo, na wewe unasema hapana, na kufanya yote mimi mwenyewe, basi jua kuwa wakati mwingine ukiwa na haja ya msaada, hawawezi kukusaidia na kukuambia, tulifikiri unaweza kufanya kila kitu mwenyewe?

Si jambo baya wakati watu wanajaribu kuwa msaada kwako kwa manufaa yako na kukupa mikono yao (give you their hands), muda wao na nguvu zao. Katika hali yoyote kama iwe kazini, nyumbani, jambo la kihisia, kimwili, au kitu unachohitaji. Kama hutaki kuuliza, huwezi kujua jibu. Pia kama watu wanakuuliza, mara zote kuwa na heshima unapouliza au kuulizwa. Daima sema, Ndugu, Naweza kukupa msaada kwa hili au haya? Tafadhali nisaidie! au asante mara nyingi utajibiwa hivyo, kwa kufanya hivyo utaona matokeo makubwa sana katika maisha yako.

Vilevile kama mtu ana tatizo gumu la kihisia (stress), huyu mtu anahitaji rafiki au mtu wa kumfariji, mtu huyo atamwambia rafikiye Naomba ushauri juu ya nini cha kufanya katika hali niliyonayo? Si unaweza kunishauri? Kamwe usisite kuomba msaada wakati unahitaji kusaidiwa. Najua inawezekana kuwa ni kitu ambacho watu wengi wana hofu ya watu, lakini unatakiwa kuondoa hofu, kusaidiana kupo daima. Unachotakiwa ni kuuliza tu.

Baadhi ya watu wana kiburi na hivyo kujiona wako juu na wenye nguvu, lakini kwa ndani au kimoyomoyo wanajua fika kwamba wanahitaji msaada, lakini wao hujaribu na kujikakamua kufanya kila kitu kusudi wasipate aibu ya kuuliza. Yaani wanajua wazi ni jambo gumu, lakini wanaamini kuwa wataweza. “Tafadhali” na “Asante” ni maneno ya kichawi. Baadhi ya watu  hata hawewezi kusema asante kwa mtu au watu ambao wamewasaidia au wamefanya mengi kwa ajili yao.

Tafadhali na Asante ni muhimu na maneno mazuri tena ya hekima na busara pia huleta baraka. Ni muhimu sana kutumia maneno haya katika kila kipengele. Hivyo omba msaada leo. Usiogope. Hakuna aliye mkamilifu. Sote hufanya makosa, sote huwa na tofauti, lakini jambo moja unapaswa kujua, msaada si kitu kibaya. kwa mtu yeyote au kitu chochote. Jaribu kujifunza kuomba msaada na kutoa msaada hakika utaona mwenyewe umuhimu wake.   Left hug Right hug


Mwandishi wa makala hii anapatikana pia:

fb Facebook        twitt  Twitter            linkLinkedIn


Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s